Kwa maoni yangu, PPRA wamefanya mengi mema na wanastahili pongezi kwani kabla ya hapo, hali ilikuwa mbaya zaidi. Sheria inakipengele cha local preference na kinatumika vizuri, japo kinatugharimu maana kwenye miradi mikubwa pale tunapotumia hii sheria kumpa "mzawa". Lakini ni bora tukubali hiyo gharama tujenge uwezo wa watu wetu. PPRA wamewezesha tenders kuwa wazi kwa kila mtu-tatizo letu sisi ni uvivu wa kujaza yale madocument makubwa ila nasi tuhsindane na wenzetu-tunaishia kulipua mataokeo yako tunakuwa-non -responsive-kisha tuaanza mjaungu! Ni vema tupongeze pale panapostahili na tuwaelekeze wapi wakaze buti kuboresha, tuache kulalamika tu kila siku jamani.