Kama una pesa ya kutosha powertiller nzuri ni Siam kubota ina 14 HP. Kama una mtaji mdogo nunua za kichina ambazo nazo ni long hand na zina 14 HP.
Hizi za mikono mifupi ni zina majembe mazito pia ni nzito mno hata utumiaji lazima kuwa watu zaidi ya mmoja wakati wa ufungaji wa majembe.
Wakati hizi za mikono mirefu ni nyepesi hata majembe yake ni mepesi, mtu mmoja tu anaoperate. Vile vile hizi za mikono mirefu hufanya kazi kwa uharaka zaidi.