Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na vipindi vya michezo ya kwenye radio, kama vile, Mahoka (Na kicheko chake, mama mbavu zangu x2 eh eh eh eh eheeeeeeeeeeeeeeeeeH AAAH) na Pwagu na Pwaguzi...!
Kuna mchezo mmoja wa Pwagu na Pwaguzi, walianzisha mradi wa zahanati ya kungoa meno huku wakiwa hawana mafunzo yoyote ya udaktari wa meno, nje ya ofisi yao waliweka bango kubwa likionesha kuwa wao ni wataalamu wa kungoa meno.
Mteja akifika anapokewa mapokezi na mwenzake Pwaguzi, baada ya kulipia pesa ya matibabu anakwenda chumbani aliko Pwagu na kuanza kungolewa meno kwa kutumia koleo za mafundi baiskeli, Ah ah ah ah.
Issue inakuja kwenye kuulizia fedha ambazo mteja alitoa, Pwaguzi siku zote alikuwa anamdhurumu mwenzake, uwa anadai kuwa zilishapotea katika purukushani za kukimbia...!
Nakumbuka kuna mradi mwingine, walikuwa wanakusanya damu za mbuzi, na kuzipeleka Hospitali, eti wanadai wanatoa msaada kwenye benki ya damu, ah ah ah ah. Hawa jamaa walikuwa mwisho.
Nawakumbuka magwiji wa michezo ya kuigiza yaani maselebu wa ukweli, kama Marehemu Mzee Hamis Tajiri (Janja au Meneja Mikupuo), Marehemu Bi Tunu Mrisho (Mama Haambiliki), Mwanaheri Ngandu, Justin Kilumbi, Ali Manjunju (Ngosha), Marehemu Mzee Batholomeo Milulu (Masawe) na Marehemu Mzee Ibrahim Raha (Mzee Jongo) Mzee Fundi Said (Kipara) na wenginewe nimewasahau.