SHEKH WA MADRASA AWABAKA WATOTO WA MIAKA 7 WANAFUNZI WAKE
Mwalimu wa madrasa ya dini ya kiislam MWANDEGE (PWANI) Mwenye miaka 39 amefikishwa polisi na wazazi wa watoto wawili (majina yanahifadhiwa )kwa kosa la kuwabaka watoto wawili hao pindi walipokuwa wakihudhuria elimu ya dini (Kiislamu) jioni katika eneo la mwandege mkoani pwani.
Wakieleza tukio hilo watoto hao walidai kuwa shekhe huyo alikuwaakiwapeleka kwake na kisha kuanza kwa kuwaingizia vidole katika sehemu zao za siri hadi pale alipohakikisha kuwa njia imeanza kupatikana. Pamoja na maumivu makali waliyokuwa wanayapata walikatazwa kusema kwa wazazi wao kwa madai kuwa endapo wataongea tukio hilo atawasomea DUWA na watakufa hivyo watoto wakakaa kimya.
Kugundulika kwa uovu huo kunatokana na mtoto mmojawao baada ya kutoka madrasa jioni alirudi akidai mamivu makali na tumbo kuuma sana kiasi cha kushindwa kutembea, wakati mama yao akimwogesha ili ampeleke hospital aligundua kuwa mtoto alikuwa ameingiliwa kimwili baada ya kumbana ndipo alipoeleza kuwa ni mwalimu wao wa madrasa kambaka.
baada ya kubaini wazazi walilazimika kuwafikisha polisi watoto hao na kuandikiwa PF3 na walipofikishwa hospital daktari amethibitisha kuwa wameingilia na wameharibiwa sana.
Pamoja na mtuhumiwa kukamatwa Jana jioni kuna taarifa kuwa amepewa dhamana kutoka kituo cha polisi suala ambalo hadi sasa linaibua utata kuwa je mtuhumiwa wa ubakaji anaweza kupewa dhamana na kuwa huru kwa muda Fulani au ni kwa sababu mtuhumiwa anatoka katika familia yenye uwezo?
Wanasheria naomba mawazo yenu ili kumusaidia wazazi hao haki iweze kupatikana maana hajui kipi cha kufanya.
Kwa mawasiliano zaidi piga
0713059054
[h=2]Tuesday, September 10, 2013[/h]
[h=3]Sheikh abaka mtoto wa miaka 8[/h]
KIONGOZI wa msikiti wa Masjid Maftah ulioko Misufini katika manispaa ya Morogoro, Alhaj Abdul Wazir, maarufu kama Sheikh Koba, anashikiliwa kwa mahojiano mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka nane, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Sabasaba.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, zilisema mtuhumiwa huyo, anadaiwa kutenda tukio hilo chumbani kwake, Septemba tatu, majira ya saa mbili usiku, huko Mbuyuni katika manispaa ya Morogoro.
Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumzia mazingira ya tukio hilo, walidai kuwa Alhaj Koba, amekuwa akiishi nyumba tofauti na mkewe na kwamba siku ya tukio mke wake alimtuma mtoto wa nduguye kupeleka chakula kwa mumewe, lakini alichelewa kurudi, hivyo kuamua kumfuatilia kujua kulikoni.
"Alipofika kwenye nyumba anayoishi mumewe, aligonga na kumuulizia binti huyo, lakini alielezwa kuwa alishaondoka eneo hilo, lakini mtoto alijitokeza na kudai alikuwa bado ndani ya nyumba hiyo, na alipohojiwa kuhusiana na uchelewaji wake, alikiri alikuwa amebakwa hivyo tukio hilo kuripotiwa polisi," kilieleza chanzo chetu cha habari.
Polisi walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.