Posho ya usumbufu na posho ya kujikimu

Posho ya usumbufu na posho ya kujikimu

BWANA MISOSI

Member
Joined
Feb 11, 2020
Posts
39
Reaction score
25
Habari za saa hizi wanaJF.

Naomba kujua, unapohamishwa kikazi bila kuomba kwa mtumishi wa umma, ni stahiki zipi inatakiwa kulipwa?

1. Kuna posho ya usumbufu
Hii inatolewa unapotoka au unapoenda?

2. Pesa ya kujikimu kwa muda gani?
Hii inatolewa unapotoka au unapoenda?

Au Kama kuna stahiki zingine kwa anayefahamu anijulishe.

Asanteni.
 
Ya kujikimu sidhani, ila utalipwa ya usumbufu ambayo ni amount fulani ambayo ipo delivered as pacentage of salary kisha inazidishawa na kilimeters to cover times mke na watoto kama wapo kwenye file ofisini.
 
Posho ya usumbufu utalipwa kwenye kituo unachohama kama sijakosea ni asilimia 10 ya mshahara wako mwaka mmoja.

Posho nyingine zifuatazo utalipwa kituo unachohamia
Posho ya kujikimu ni posho ya siku kumi na nne viwango vyake vinatofautia kwa cheo na sehemu Kama ni jiji manispaa au wilayani hi inalipwa kwa mtumishi mwenza wake na watoto 4.

Pia kuna posho ya njiani Kama umesafiri zaidi ya masaa 6 ambayo ni nusu ya perdiem yako ya siku na italipwa kwa mtumishi , mwenza wake na watoto pia kuna malipo ya nauli ulizotumia kusafiri hapa tiketi zitahusika.

Kuna posho za kusafirisha mizigo tani zinatofautiana kulingana na cheo Cha ko na zinalipwa kutegemea umbali kwa kilometa kutoka kituo ulichohama hadi kipya inalipwa sh 1000 kwa kilometa kwa tani 1

Kama unagari binafsi utatakiwa kulipiwa millage za kuhamisha gari lako
Huko serikalini ukihamishwa kama unacheo kikubwa na unafamilia kubwa na unahamishwa umbali mrefu let's say kutoka musoma hadi ruvuma unaweza Jenga nyumba ya kawaida ikakamilika Kama unakiwanja tayari
 
Posho ya usumbufu utalipwa kwenye kituo unachohama Kama sijakosea ni asilimia 10 ya mshahara wako mwaka mmoja.

Posho nyingine zifuatazo utalipwa kituo unachohamia
Posho ya kujikimu ni posho ya siku kumi na nne viwango vyake vinatofautia kwa cheo na sehemu Kama ni jiji manispaa au wilayani hi inalipwa kwa mtumishi mwenza wake na watoto 4.

Pia kuna posho ya njiani Kama umesafiri zaidi ya masaa 6 ambayo ni nusu ya perdiem yako ya siku na italipwa kwa mtumishi , mwenza wake na watoto pia kuna malipo ya nauli ulizotumia kusafiri hapa tiketi zitahusika.

Kuna posho za kusafirisha mizigo tani zinatofautiana kulingana na cheo Cha ko na zinalipwa kutegemea umbali kwa kilometa kutoka kituo ulichohama hadi kipya inalipwa sh 1000 kwa kilometa kwa tani 1

Kama unagari binafsi utatakiwa kulipiwa millage za kuhamisha gari lako
Huko serikalini ukihamishwa kama unacheo kikubwa na unafamilia kubwa na unahamishwa umbali mrefu let's say kutoka musoma hadi ruvuma unaweza Jenga nyumba ya kawaida ikakamilika Kama unakiwanja tayari
Kama umehama ndani ya wilaya moja je? Kuna gharama ya kujikimu n.k unalipwa?
 
Asante kwa ufafanuzi. Kwa hiyo nikitaka kudai hizo pesa za usumbufu nilikotoka nafanyeje? Naandika barua? Kuna haja ya ku-note vitunguu vya sheria kwenye barua hiyo? Naomba Kama kuna uwezekano wa kupata kifungu cha sheria ili inisaidie kufuatilia hilo.
 
TMAA Washushwe
Acha Kuuliza Sana Utashushwa
 
Back
Top Bottom