Posho posho posho

Magehema

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
428
Reaction score
28
Ni mjadala wa posho, umetawala kurasa,

Taka kutoana “roho”, kwa hoja zinazotesa,
Tena sio za kitoto, hoja wameitakasa,
Nini uhalali wake, jifungu hilo la posho?

Embu fanya tafakuri, tumia zako busara
Sitangulize kiburi, mwishowe pata hasara,
Tupangie mistari, bila kufanya papara,
Nini uhalali wake, jifungu hilo la posho?

Mtu tusimhakiki, hojaye tuijadili,
Tuipime mantiki, tumie zetu akili,
Tuepuke urafiki, tunapoitafakali,
Nini uhalali wake, jifungu hilo la posho?

Katika shilingi mia, thelathini za miradi,
Sabini zilobakia, posho tunajiahidi,
Wananchi waumia, viongozi wafaidi,
Nini uhalali wake, jifungu hili la posho?

Wale mnaoziunga, tupeni zenu sababu,
Msisingizie unga, malazi na matibabu,
Au fenicha kuchonga, embu nipeni majibu,
Nini uhalali wake, jifungu hili la posho?

Kuna mmoja kasema, posho zinahamasisha,
Mdomowe waachama, bila posho amekwisha,
Hatoweza kujituma, mzigo ataushusha,
Hao ndio viongozi, tulowapigia kura.


Kuipamba hoja yake, kahusisha wananchi,

Wale wa jimboni kwake, kuwapoza hakuishi,
Si msiba si sherehe, lazima akate pochi,
Kazi mpya ya mbunge, ndio kwanza nasikia!

Kuna mengi kukwambia, muhimu kutafakari
Wengine kusinzia, au kupiga stori,
Mihayo wajipigia, wameshashiba mtori,
Bado wanataka posho, ikibidi iongezwe.

Embu nawe endeleza, japo ubeti mmoja,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…