Porojo za bongo

Bwana Bongo

Senior Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
167
Reaction score
239
Nikiwa napitia kitabu chenye jina la kiongozi, ambacho kinajulikana kihistoria kama The Prince, kilichoandikwa na Niccolò Machiavelli mnamo karne ya 16, nilikutana na hoja zilizofanya nianze kutafakari kwa undani hali ya uongozi na mabadiliko ya mamlaka. Kitabu hiki ni miongoni mwa kazi muhimu zaidi katika historia ya siasa, kikitoa maelezo ya uhalisia kuhusu namna viongozi wanavyopata, kudhibiti na kupoteza madaraka. Katika kitabu hiki mwandishi anagawa aina za uongozi, zikiwemo tawala za kifalme na za kijamhuri, na anaeleza tabia za watu na mizizi ya changamoto katika mifumo ya utawala.

Jambo lililonishangaza lilikuwa kukutana na maneno yake akisema kwamba, “Watu wanaotaka kuboresha maisha yao, mara zote wako tayari kubadili mtawala kwa matarajio ya maisha bora; watabeba silaha na kuasi dhidi ya kiongozi yeyote. Lakini hili huwa ni kujidanganya tu, na uzoefu unaonyesha kuwa huwa wanajikuta katika hali mbaya kuliko hapo kabla.

Hili linatokana na hali ya asili, nayo ni kuwa kiongozi mpya hawezi epuka kuwakwaza raia wake.” Katika maelezo haya, Machiavelli anaonesha kuwa wananchi mara nyingi huingia katika mtego wa matumaini makubwa, wakifikiri kuwa mabadiliko ya uongozi ndiyo njia ya haraka ya kuboresha maisha yao. Hata hivyo, mabadiliko haya huja na gharama, na huwa yanahusisha kipindi kigumu ambacho wananchi huathirika zaidi kuliko wanavyotarajia.

Kwa mujibu wa hoja hii, inamaanisha kuwa yale yanayohitajika na wananchi katika awamu ya uongozi mpya hayawezi kupatikana mara moja. Hata hali ya nchi haiwezi kuwa kama ilivyokuwa hapo awali kwa sababu mabadiliko ya taasisi, mifumo na uongozi husababisha misukosuko ya mpito. Machiavelli anaendeleza hoja hii kwa kusema kuwa, “Mambo mengine yanayoweza kutokea ni maudhi aliyotenda wakati anaposimamisha utawala mpya. Hapo atajikuta kajenga maadui pande zote. Wananchi wanamdai, uongozi uliondolewa utamdai.” Katika hali hii, kiongozi mpya hukutana na upinzani kutoka kwa pande zote: wale wanaotaka mabadiliko ya haraka na wale waliokuwa na maslahi katika utawala uliotangulia. Hivyo, kwa mtazamo wa Machiavelli, kiongozi mpya huwa kwenye hatari kubwa zaidi kuliko kiongozi wa zamani aliyekwishaimarisha nafasi yake.

Hatimaye, anafunga hoja kwa kusema, “Nchi ikiasi na uasi huo ukazimwa, ni vigumu sana kuasi tena na kufanikiwa. Sababu ni kuwa mtawala atatumia uasi huo kama sababu na kisingizio, na kwa kisingizio hicho hata sita kujilinda kwa kuwaadhibu vikali wale wanaompinga. Atawahukumu washukiwa na hivyo kujiimarisha katika maeneo ambayo alikuwa dhaifu.” Kauli hii inaonesha kuwa jaribio la uasi lisilofanikiwa mara nyingi huimarisha zaidi mamlaka ya mtawala kuliko kuudhoofisha. Kwa kutumia uasi kama sababu ya kuongeza ukali, kuongeza nidhamu na kuadhibu wapinzani, mtawala hutengeneza mazingira magumu kwa watu kuasi tena. Hili linatoa picha ya uhalisia kwamba nguvu ya utawala mara nyingi hutengenezwa baada ya misukosuko, si kabla yake.

Kwa jumla, mawazo ya Machiavelli katika kitabu hiki yanaonesha kwamba mabadiliko ya uongozi si jambo jepesi kama watu wengi wanavyodhani. Wananchi husukumwa na matumaini, lakini viongozi wapya hukumbana na uhalisia mgumu unaohitaji maamuzi magumu na mara nyingi yanayokera. Hivyo, kitabu hiki kinaendelea kuwa rejea muhimu katika kuelewa siasa, mabadiliko ya madaraka na tabia ya binadamu katika mazingira ya utawala.

#wamakamo ✍️
 
Niccolò Machiavelli mnamo karne ya 16, nilikutana na hoja zilizofanya nianze kutafakari kwa undani hali ya uongozi na mabadiliko ya mamlaka.
Niccolo Machiavelli aliandika hivi ili wananchi waridhike na wakoloni na walio jimilikisha watumwa. Ili wabaki kuwa watumwa na wananchi wabaki kuikubali serikali iliopo madarakani.

Na walio madarakani na kumiliki watumwa wazidi kutajirika kwa unyonge wa wananchi na watumwa.
 
Uhalisia gani, upupu mtupu!
Uwo sasa ni mtazamo wako siwezi kubishana na wewe
Niccolo Machiavelli aliandika hivi ili wananchi waridhike na wakoloni na walio jimilikisha watumwa. Ili wabaki kuwa watumwa na wananchi wabaki kuikubali serikali iliopo madarakani

Lakini mifano ipo na imeitoa wazi wazi
 
ila kama mtu haeleweki nk vyema atolewe huwezi vumilia mtu anakupeleka shimoni ww umekaa tu kama vUz!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…