Pongezi ziwaendee vijana wawili ninaowafahamu vizuri sana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
PONGEZI KWA POLEPOLE NA HAPI!

Ziwaendee vijana wawili ambao nawafahamu vizuri, Humphrey Polepole na #Salum_Hapi, kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya.

Humphrey ni mstahimilivu, anayejenga sana hoja na anayejifunza kuwa na busara. Hapi ni mwanaharakati mwenye misimamo katika masuala ambayo ameyapa kipaumbele na nimemfahamu tangu tukiwa Chuo Kikuu.

Wawili hawa wanafanana kwa jambo moja, wanaweza kusimamia jambo hadi mwisho wakitaka. Tofauti yao ni kuwa Humphrey anajua vitu vingi zaidi na ni mbunifu zaidi.

#MY_TAKE;
Wakati wengi wetu tunautizama uteuzi huu kama “Business as usual”, mimi nautizama kama mkakati wa muda mrefu wa CCM kuwajenga vijana na kuwaandaa kikamilifu kuvaa viatu vya wazee, CCM hujiandaa muda mrefu sana na upinzani una tabia ya kufanya maandalizi ya dakika za mwisho na ya zimamoto na wakati mwingine hata kusubiri nani ameachwa CCM ili apewe nafasi(Hii haimaanishi kuwa Upinzani hauna rekodi ya kuandaa vijana)

Msisitizo wa hoja yangu ni kuwa, JPM amekuja na mkakati muhimu, anatafuta vijana wenye uelewa mkubwa sana na wenye uwezo mkubwa wa kuleta changamoto kwa upinzani.. Vyama vya upinzani visipokuwa makini na vikijiendesha kimazoea vitajikuta kwenye wakati mgumu kwa sababu ma-DC vijana aina ya Polepole, Hapi na kama wataendelea kuteuliwa vijana CREAM ya aina yao - hawawezi kuwa sawa na wale waliokuwa wanateuliwa awamu iliyopita kwa sababu za kirafiki na kimtandao zaidi.

Nihitimishe hoja yangu kwa kukumbusha kuwa teuzi za namna hii ni KITISHO kikubwa cha ushindani dhidi ya UKAWA siku za mbele. Vyama vya UKAWA pia vijipange sana na viendelee kuwafunza na kuwatunza vijana wenye uwezo (CREAM YOUTHS) ili ku-balance mkakati wa JPM na CCM juu ya jambo hilohilo, ikiwa ni pamoja na kuwaamini kwenye majukumu makubwa kwa ajili ya siku za mbele.

Ukiona mwenzio anajipanga kwa mikakati ya muda mrefu, usiidharau na ifanyie kazi kwa sababu uongozi wa dunia hivi sasa unahama kwa nguvu kutoka kwa wazee kwenda kwa vijana.

Niwatakie asubuhi njema na tafakuri makini.

Mtatiro JPONGEZI KWA POLEPOLE NA HAPI!

Mtatiro J
 
Leo Mtatiro kasema kweli...,vyama vya ukawa havina "succession plan"..vimetengeneza miungu....Cuf hawana mpango na kujenga chama bara...chadema hawana mpango kwenda zanzibar..Salum Mwalim,NKM Zanzibar yupo Dar kila siku.

Chadema wameruhusu watu wasio na itikadi nawageni wenye ukwasi kukihodhi...hili litafunuka uchaguzi mkuu wa chama,vijana wenye itikadi ya siasa za chadema wametupwa..."kundi"..jipya linaundwa...ndani ya chama.Watu wenye mvuto kama kina Kagaila chalii...hii inajengwa..kuuwa taswira ya chama.Siasa ni sayansi....haya yote yameletwa na siasa za tumbo.
 
very true upinzani nadhani waasione aibu kuiga vitu vizuri kutoka ccm wajifunze tu maana hawa jamaa ni wakongwe na wanajua kuicheza hii ngoma siasa za kushitukiza zitaendelea kuleta malalamishi tu kila siku kutoka upinzani na wa invest pia vijijini wajitahidi kupata fungu kuanzia sasa waanze kuenea vijijini, maana ndio style ya ccm wanasema kuisha kwa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine lakini upinzani kuisha kwa uchaguzi ndio likizo ya kula zile hela za uchaguzi kwenda holiday.
 
Hivi ile amri ya kuzuia shughuli na mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani ni ilitolewa na Mheshimiwa nani vile?
 
Hata hivyo ningeshangaa sana kwa kelele zile zote Polepole alizukuwa anazipiga kama asingetunukiwa asante hii aliyopewa...Ila toka Serikali iliyopita cheo hiki cha ukuu wa wilaya kimekuwa kikitolewa kama kuwalipa fadhila baadhi ya watu kwa maslahi ya mkuu tu..
 
☝Kulinganisha vijana wa CCM na upinzania ni kujionea. Ni nafasi gani katika upinzani inafanana na ukuu wa wilaya? Siasa za upinzani ni siasa za mapambano na za kujinyima fursa za kufaidi wakati zile za CCM ni za fursa za kupata kazi na fursa za kimamlaka. Inahitaji bidii kuvutia vijana waliosoma kujiunga na upinzani wakati vijana wa CCM wanakesha wakijinadi huko ccm ili wapate fursa za kuteuliwa. Tafadhali sana tusilinganishe njugu na mawe!

Prof. Kitila Mkumbo
 
Back
Top Bottom