Pongezi sana Kwa Halima Binti wa Bakari Bulembo, Atakuja Kutisha, Mark My Words

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mimi sio Mpenzi wa CCM hata Kidogo. Ila Nimeona Sio Vibaya Kumtia Kijana huyu Moyo. Mara Nyingi huwa Nikimsikiliza Mtu Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kiakili na Kiuongozi Naweza Kumgundua Mapema. Kuna Kabinti Fulani Bungeni, Nafikiri Ni Yule Mtoto wa Bakari Bulembo. Huyu Mtoto anakipaji Kikubwa sana cha Kujieleza na Kujenga Hoja. Naamini kwamba atakuja Kuwa Mwanasiasa Mwanamke Maarufu Tanzania, Hilo halina tena Mjadala.



Mojawapo ya Sifa Kubwa ya Mtu Mwenye Uwezo wa Kujieleza (argumentation) Anazungumza Kwa Mifano halisi, anarejea Historia, Anatoa Mifano ya Kugusa! Na anatoa Takwimu na Vigezo, Na Kama Swala Lenyewe Ni La Kitaalamu analitetea kwa matokeo ya Tafiti Na Huyu Mtoto yote Anayazinatia.

Ila Ushauri Wangu Ningemtahadhalisha Mapema, Ajiepushe na Siasa za Maji Taka, Ngojera na Hadaa Kama akina Kibajaji na Nape. Ajikite zaidi Kwenye Hoja zenye Maslahi ya Taifa. Bila Kuwa Mzandiki. Atahshimika na Atatisha Kila Upande lakini akileta Ngojera na Uzandiki, atadharaulika Bado mdogo na Ndio Basi.

Pongezi sana Mwanangu Halima Bulembo, Keep it Up
 
Huyu Hapa Picha yake Na Hii ni Mojawapo ya hoja zake!
rUjc6teO.jpg


 
Hoja gani muhimu aliyojenga hapo mbali na kunakiri na kunukuu tafiti zilizofanywa na taasisi mbali mbali kuhusu elimu yetu. Kung'ang'ania kutaja hizo namba ndiyo kujenga hoja?

Naona mleta mada una ajenda yako binafsi ya kumpiga jeki huyo binti au una maslahi binafsi naye.
 
KUna baadhi ya budget allocations hatuwezi kuigawa tu kwa percentage... vitu kama ulinzi, miundombinu, mawasiliano, kilimo nk haviwezi kuwa segregated kwa namna ambavyo huyu binti anataka... pia si vibaya kumpa shule ya some fixed parameters na variable parameters kwenye kutengeneza budget

Safari ya kumfunza na kumfunda huyu binti ni ndefu na sina hakika kama ni sharp... hasa baada ya kauli mbofu kama ile ya kuhusu bunge lisiwe live
 
Back
Top Bottom