Pongezi na ushauri kwa waziri January Makamba

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,875
Heshima kwako waziri na wizara kwa ujumla!

Baada ya salamu hizo napenda kukupongeza kwa nia yako ya dhati ya kuondoa viroba sokoni. Pombe hii ilikuwa inaharibu sana vijana wenzetu, wazazi wetu na watoto wa shule. Viroba ilikuwa na bado ni janga la taifa letu, ulikuwa unakutana na mtu anatembea kumbe ana pombe mfukoni, hii hali ilikuwa anaangamiza taifa letu.

Ndugu waziri naomba sana ufanye haraka iwezenakavyo kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya nailoni. Hii mifuko inaharibu mazingira sawa sawa na mifuko ya kufungia hiyo pombe kali inayoitwa viroba. Ndg waziri mifereji yetu kwenye miji mbalimbali yamezibwa na hii mifuko ya nailoni, mitaa imechafuka na uchafu mkubwa ni hii mifuko.

Nakuomba usiangalie nyuma katika kupiga marufuku mifuko tajwa. Wenye viwanda watafute technolojia nyingine yenye uwezo wa kutengeneza mifuko rafiki kwa mazingira yetu. Kweli viwanda tunavitaka sana maana tuna shida na kodi na ajira ila si kwa gharama ya mazingira yetu.

Nashauri serikali iwekeze kwenye kuwapa elimu vikundi vya wajasiriamali wa kutengeneza vikapu , wapewe elimu ya kutengeneza vikapu vya size tofauti na kisha wananchi wahimizwe kuvitumia kubeba vitu mbalimbali vinzvyohitaji mifuko. Hapa tutakuwa tumeokoa mazingira lakini tutakuwa tumewapa mama zetu ajira.

Hata kiuchumi itakuwa nafuu maana kama kikapu kitauzwa hata elfu tatu na itadumu kwa muda bado ni nafuu kuliko hii mifuko inayouzwa kuanzia shilingi 50 hadi 2000 na haina uwezo wa kukaa siku nyingi. Ndg waziri hebu wape wenye viwanda hivi muda ili wahakikishe mzigo wao unaisha na baada ya hapo hii mifuko ipigwe marufuku. Wakati huo huo weka mpango wa kuhamasisha matumizi ya vikapu vyetu vya asili.

Naomba kuwasilisha kwako , nakutakia kazi njema.​
 
Waziri Makonda ndo waziri gan tena mkuu mi ata sijasoma post yako aseeeee
 
Waziri Makonda ndo waziri gan tena mkuu mi ata sijasoma post yako aseeeee
Aisee hujaona sorry yangu? halafu naona ni kwasababu almost one week kila nikiingia humu nakumbana na upepo mbaya unaovuma kuelekea kwa mkuu wetu wa mkoa.
 
Back
Top Bottom