Pongezi kwa TANESCO Mwanza

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,679
2,000
Pamoja na madhaifu yote mliyonayo lawama nyingi tunazo walaumu.lakini mwisho wa siku ule usemi wa "mnyoge mnyogeni lakini haki yake mpeni " unatimia.
Leo mida ya SAA kumi na nusu jioni hivi,transformer ya maeneo ya Igogo huku VOIL ililipuka.kwa hiyo kazi zote za umeme zilisimama,mfano wachomeleaji na zingine.na tukajua hapa umeme hadi siku tatu hivi ndio utakuwa sawa. Kwani ndivyo tulivyozoea.cha kufurahisha yaani kabla ya saa nne usiku tayari umeme umewaka kama kawaida.
KWA HILO UKWELI NAWAPA PONGEZI KWA KAZI NJEMA SANA
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,751
2,000
Itakuwa kuna Kigogo alivyoona mambo yake yamesimama kaenda kuwapa Michuzi wake fasta sio kuwa wameguswa na Shida zenu
 
Majestic wolf

JF-Expert Member
Feb 10, 2015
1,245
2,000
Ni kweli Tanesco siku hizi wanajitahidi mnaoponda utakuta hata hitilafu ya umeme hamjapata sema basi ndo hivo tu kupondea
 
Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,716
2,000
Ni kweli Tanesco siku hizi wanajitahidi mnaoponda utakuta hata hitilafu ya umeme hamjapata sema basi ndo hivo tu kupondea
Ongea ujuavyo hilo shirika ni chafu linatakiwa kusafishwa kwanza bei kubwa ya umeme na kukatika ni muda wowote...
 
TangataUnyakeWasu

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,276
2,000
Pamoja na madhaifu yote mliyonayo lawama nyingi tunazo walaumu.lakini mwisho wa siku ule usemi wa "mnyoge mnyogeni lakini haki yake mpeni " unatimia.
Leo mida ya SAA kumi na nusu jioni hivi,transformer ya maeneo ya Igogo huku VOIL ililipuka.kwa hiyo kazi zote za umeme zilisimama,mfano wachomeleaji na zingine.na tukajua hapa umeme hadi siku tatu hivi ndio utakuwa sawa. Kwani ndivyo tulivyozoea.cha kufurahisha yaani kabla ya saa nne usiku tayari umeme umewaka kama kawaida.
KWA HILO UKWELI NAWAPA PONGEZI KWA KAZI NJEMA SANA
Kwani ww unafikiri wao wajinga wanataka kutumbuliwa??
 
masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,679
2,000
Ni kweli Tanesco siku hizi wanajitahidi mnaoponda utakuta hata hitilafu ya umeme hamjapata sema basi ndo hivo tu kupondea
Kwenye madhaifu tunasema lakini pia wanapifanya vizuri pia tuseme... Ukweli kwa sehemu yangu Leo wamenifurahisha sana...
Siku hizi hata saa tano usiku huwa wapo wanafanya kazi..
 
masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,679
2,000
Itakuwa kuna Kigogo alivyoona mambo yake yamesimama kaenda kuwapa Michuzi wake fasta sio kuwa wameguswa na Shida zenu
Mkuu,mtaa wa igogo hakuna kigogo huku, labda Wewe co mwenyeji wa mwanza
 
masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,679
2,000
Ujue hiyo mitaa kuna kigogo anaishi.. Hawa si watu unazungumza Transifomer wakati nguzo tu siku 4 hapa kwetu Kiloleli
Labda haujawahi sikia sifa za igogo..hakuna hata KIGOGO anayefikilia kukaa huku
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,751
2,000
Mkuu,mtaa wa igogo hakuna kigogo huku, labda Wewe co mwenyeji wa mwanza
Hakuna Mtaa usio na Kigogo Ila Kigogo wa huko hafanani na wa kwetu,

Hata Seaview kuna Maskini wa Mtaa japo kwa Igogo huenda ndo akawa Mshua!
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
173,757
2,000
Kuna watu raha yao ni kujiropokea tu hata kwa jambo wasilolijua ili mradi tu wapate amani ya moyo kupinga mazuri ya kitu husika.
Mkuu,mtaa wa igogo hakuna kigogo huku, labda Wewe co mwenyeji wa mwanza
 
  • Thanks
Reactions: lup

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom