singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SERIKALI imeongeza bajeti yake ya kununua dawa kutoka Sh bilioni 41 kwa mwaka 2014/15 hadi Sh bilioni 251 mwaka huu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema lengo la hatua hiyo ni kudhibiti uhaba wa dawa nchini. Waziri huyo mwenye jukumu hilo nyeti aliyasema hayo mjini Kahama mkoani Shinyanga, wakati akizungumzia upatikanaji wa dawa nchini baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya kupima Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa wasichana.
Ummy anasema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli itahakikisha kuwa hakuna mgonjwa atakayekufa kwa kukosa dawa, kwani katika bajeti ya mwaka huu serikali imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya kununua dawa.
Kwa dhati kabisa nachukua fursa hii kuipongeza serikali kwa hatua inazoendelea kuzichukua katika kutatua matatizo yanayowahusu wananchi masikini wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na matatizo yanayohusiana na sekta ya afya.
Hata kabla ya kutangaza ongezeko hilo la bajeti kwa ajili ya ununuzi wa dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao, serikali ya awamu ya tano, tayari ilikuwa imeshaanza kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na matatizo yanayohusu sekta ya afya ambayo ni sekta nyeti kutokana na kuhusisha afya ya nguvu kazi moja kwa moja.
Mara tu baada ya kuingia Ikulu, Rais Magufuli alianza kuchukua hatua za dharura za kutafuta fedha ili kuanza kushughulikia matatizo katika sekta hiyo, hasa pale alipoanza kuhamisha fedha zilizotengwa kwa matumizi mengine na kuzielekeza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kununua vitanda na hata dawa.
Kama vile haitoshi serikali katika kipindi hicho cha mwanzo kabisa cha uongozi wake, ilitoa agizo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuanza kufungua maduka ya dawa katika hospitali kubwa nchini na kupiga marufuku maduka ya dawa ya binafsi nje ya majengo ya hospitali za umma, hatua iliyolenga kudhibiti biashara ya magendo katika dawa na pia kushusha bei za dawa kwa wagonjwa.
Licha ya maagizo hayo, Waziri mwenye dhamana na sekta ya Afya, Ummy na Naibu wake, Dk Hamis Kigwangallah walianza ziara za kushtukiza katika hospitali mbalimbali nchini na kuangalia mifumo ya uendeshaji wa hospitali hizo, hatua ambayo kwa kiwango kikubwa imewezesha huduma kutolewa kwa uhakika kuliko nyuma.
Kwa hatua ya sasa ambapo udhibiti wa dawa za serikali umekuwa mkubwa, ikiwa ni pamoja na dawa hizo kuwekwa nembo ya serikali, ni hakika kwamba ongezeko hilo la dawa litakwenda kuwasaidia wananchi wengi masikini, na hivyo afya za wananchi zitaimarika na hivyo nguvu kazi kwa taifa na hasa maeneo ya vijijini itaongezeka.
Kwa dhati kabisa nimpongeze Rais na Waziri wa Afya kwa uamuzi huo, ambao unazidi kudhihirisha ahadi zake wakati wa kampeni kwamba ataipa uzito mkubwa na wa pekee suala la sekta ya afya akiwa madarakani.
Pamoja na pongezi hizo, nitoe mwito kwa mamlaka zinazohusiana na mchakato mzima kuanzia wa utengaji wa bajeti, utaoji wa fedha, matumizi ya fedha, ununuzi wa dawa na usambazaji wa dawa, kulipa suala hilo la afya umuhimu mkubwa kama ilivyoamuliwa na serikali yenyewe ili lengo hilo liweze kutekelezwa kwa asilimia 100.
Kama hilo litafanyika nina hakika matatizo tunayoyaona sasa katika sekta ya afya yanaweza kubakia kuwa historia katika kipindi cha miaka michache ijayo na Watanzania watasahau kabisa mateso ambayo walikuwa wakikumbana nayo huko nyuma walipokuwa wakikimbizana katika hospitali mbalimbali kupigania afya zao.