Malick M. Malick
JF-Expert Member
- Apr 2, 2013
- 658
- 314
Leo ni siku ya kumbukizi ya baba wa Taifa letu, Mwl Julias Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa JMT. Muasisi wa Taifa letu,
Baba wa Taifa alikua na ndoto nyingi sana kwa Taifa letu la Tanzania, zingine alitimiza ndani ya kipindi chake, zingine zilikamilishwa na waliofutia..
Baba Taifa alikua na ndoto ya Muda mrefu, ya kuhakikisha serikali inahamia Dodoma, kwa kuona kwa macho yake.. Chama cha mapinduzi kilifanikiwa kuhamia makao, ikiwepo na Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma, pamoja Wizara ya Tamisemi.
Ila kulikua na tatizo baadhi mashirika yalikua hayataki kwenda Dodoma, Ofisi za makao makuu waliendelea kujenga Dar, nakumbuka Katika mkutano mkuu wa kawaida wa CCM-October 1982, Mwalimu Nyerere aliendelea kuhoji "kwanini wakuu wa Taasisi wanaendelea kujenga majengo ya Ofisi zao kuu Dar, wakati sio Ofisi za bandari"
Kwahiyo hizo zilikua ndio baadhi ya changamoto,ikapita awamu ya pili, ya Tatu, ya Nne.. tukawa na alama kubwa mbili kuwa Dodoma ni Makao makuu ya Nchi, nazo ni Bunge, na Makao makuu ya Chama cha Mapinduzi, na zingine ndogo ni Ofisi ya LAPF, Ofisi ya Waziri Mkuu. Ila bado atukuweka miguu miwili yote..
Ilipofika awamu ya Tano, kupitia Rais wa JMT, Dr Magufuli, akafanya kwa dhamira ya dhati Katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015/20 wa serikali yake kuhamia Dodoma..
Hapo ndio inaponifanya nitoe pongezi Sana kwa Rais wetu kipenzi cha Wanyonge wa Tanzania.
Aliweka dhamira ya kweli, Katika hili hajawai kumung'unya maneno, alisema Serikali inakwenda Dodoma.. Na muongozo ukatolewa
Zilianza Wizara, na Mawaziri wao, Idara, na Taasisi, Balozi
Ikaja zamu ya Waziri Mkuu, akafuata, baada ya Waziri Mkuu kaja Makamu wa Rais,
Ukiangalia viongozi wa Kitaifa waliohamia Dodoma unaona jinsi gani dhamira ya kweli ya Rais wetu kuhamia Dodoma, hakika anastahili kupewa hongera sana kwa nia, na kuthubutu, kufanya Mambo kwa vitendo. Aja ya Mja kunena, Muungwana Vitendo, hakika unasema na kutenda Rais wetu, endelea kuchapa kazi, kwa kuonyesha njia.
Ukitaka kujua Rais wetu anachapa kazi, kabla JPM Kuingia madarakani, wanachama wa Chama cha mapinduzi walipata tabu sana kujitambulisha kama wana CCM, sababu tulikua tunatukanwa sana na wapinzani wetu
Baada ya JPM kuwa Rais, na Mwenyekiti wa CCM, tumeona na kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji, tumeona hata wale vijana waliokuwa upinzani, wakitutukana sasa hivi wana rudi nyumbani Kumenoga..
Tunaendelea kuwakiribisha Warudi nyumbani kumenoga..
Rais wetu kufanya mabadiliko makubwa, leo tunaona wabunge wa vyama vya upinzani wanaacha Ubunge na kuhamia CCM, hakika ni jambo kubwa la kumpongeza Mwenyekiti wetu na Rais wetu.. Utendaji wake umewavutia watu wengi sana ndani na nje ya Tanzania..
Kupitia siku hii muhimu ya kumbukizi ya Baba wa Taifa, nakupongeza sana kwa kuchapa kazi, na sisi huku chini tunaendelea kuchapa kazi kama Kauli mbiu Yetu ya 2015 "HAPA KAZI TU"
Ndimi
Malick Maliki