Angerudi na medali, ningeungana na wewe kumpongeza. Kinyume na hapo, namshauri aendelee kukaza msuli. Haiwezekani majirani zetu Wakenya na Waganda kila mashindano yanapo tokea, wanarudi na medali, halafu sisi tunang'aza ng'aza tu macho!
Halafu yule Filbert Bayi, hivi ni Katibu Mkuu TOC wa maisha? Kila uchaguzi unapofika, ni lazima ashinde yeye!! Huku akiwa hana tija yoyote ile!! Kwa nini asitumie muda wake mwingi kusimamia shughuli zake za kumuingizia kipato, na hiyo Kamati ya Olimpiki kuwaachia wengine?
Kha!! Yaani amejigeuza kuwa Nkurunzinza wa Kamati ya Olimpiki Tanzania!!!