Wana JF,
Mimi baada ya kutafakari kwa kina kwa ushindani uliopo na chuki inayojitokeza kati ya vyama vikuu viwili vya siasa CHADEMA na CCM nimekuja kugundua kwamba CHADEMA imeweza kufanya kazi kubwa sana ya kuidhoofisha CCM kwa mwaka 2012 na 2013 kwa kueneza sera zake zinazokubalika kwa Watanzania. Sifurahi chuki baina ya hivi vyama viwili lakini hakuna jinsi kwa sababu ndio hali halisi kuwa waliozoea kutawala baada ya kuona uwezekano huo unaweza usiwepo kabisa 2015 wameamua kueneza siasa za chuki.
Uthibitisho wa kwamba CHADEMA imefanya kazi kubwa ya kuidhoofisha CCM ni siasa za maji taka na chuki inayojitokeza baina ya vyama hivi viwili pasipo kuisahau NCCR Mageuzi. Haina shaka kwamba chuki hii ya CCM dhidi ya vyama vinzani ni hofu ya kuondoka madarakani
CCM walidhani historia ya vyama vya upinzani nchini Tanzania ya kuanza kwa nguvu na wao CCM kuvidhoofisha itafanikiwa kwa CHADEMA sasa wamekuja kugundua muda unaenda badala ya CHADEMA kudhohofika kinaimarika zaidi
Natoa pongezi kwa uongozi wa CHADEMA ngazi ya Taifa , Kanda, Mikoa , Wilaya hadi ngazi ya msingi matunda ya kazi yenu yameonekana
Nawasilisha