ashy da don
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 615
- 671
Wakuu habari za jioni humu ndani.
Najua wengi wetu ikiwemo mim tunawachukia sana askari polisi kutokana na vitendo vyao vya unyanyasaji kwa raia.
Kwa hili nililoshuhudia hapa kituo cha stesheni ningeomba nichukue fursa hii kuwapongeza sana askari hawa. Takribani ni mwezi sasa nimeukuta utaratibu ambapo polisi husimamisha madaladala yote yanayotoka Mbagala rangi tatu, na Temeke na kuwaamuru wanafunzi wapande kwanza kwa utaratibu maalumu wa kupanga mstari,na kila gari kuchukua wanafunzi takribani watano..
Utaratibu huu umenifurahisha sana kwani nikikumbuka enzi hizo nasoma Benjamin Mkapa tulikua tunasumbuliwa sana na makonda hadi kufikia hatua ya kuleta uadui kati yetu na wao.
Nachukua fursa hii Kuwapongeza jeshi letu hili la polisi na kuomba rai kwa vituo vingine kuiga mtindo huu kama polisi hawa..
safi saana, ulisoma mwaka gani mkuu. mimi pia nilisoma hapo
unaweza ukawa classmate wewe ulimaliza benja mwaka gani
aisee kumbe wameanza kuwa waungwana
unaweza ukawa classmate wewe ulimaliza benja mwaka gani
Hapana mkuu! mim nimemaliza Harvard University U.S.A! mambo ya benja mim siyajui kaka
Ni kazi nzuri na inastahili kupongezwa, ila isije tu ikawa ni mbwembwe za kuelekea uchaguzi!
Hahaa mkuu kwa hyo jamaa wanajikosha kwa ajili ya uchaguzi..
Bravo!! Wenzetu wa Nairobi hii kitu ipo toka zamani. Ingekuwa vema sana ifanyike katika vituo vyote
kweli ni la kuwapongeza...sasa maaskari mliopo humu msije mkalewa sifa na mkabadilika
Hivyo ndivyo tunavyopenda kusikia.
Kidogo kidogo tutafika tu, itafikia pia kuwapa kipa umbele wakina mama wajawazito.
Maana linapokuja suala la ustaarabu kwenye madalala kwa kweli tunashindwa, ni kugombania.
Kwa hilo nawapongezeni sana, safi