Ponda azusha mapya

Ponda azusha mapya

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,092
PONDA_85a5f.png

SAKATA la Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, limeendelea kuwa gumzo katika maeneo mbalimbali, huku matamko makali yakitolewa dhidi ya Serikali.Sakata hilo limeonekana kutikisa na kutawala vyombo vya habari, baada ya kiongozi huyo wa dini kudaiwa kupigwa risasi, kusomewa mashtaka kitandani na baadaye kupelekwa gerezani chini ya ulinzi mkali akitolewa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI).Suala hilo limeibua hisia nyingine baada ya masheikh jijini Dar es Salaam, kutoa tamko lenye mwelekeo wa kupinga udhalilishwaji wa kiongozi huyo na kuionya Serikali juu ya mwenendo huo.Mbali na masheikh kutoa tamko jana, Jeshi la Polisi kwa upande wake nalo liliimarisha ulinzi katika Msikiti wa Kichangani, uliopo Magomeni na ule wa Mtambani uliopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.hdg

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajab Katimba, alisema kitendo hicho ni kibaya kwani kinapandikiza chuki baina ya Waislamu na Serikali.Sheikh Katimba ambaye alikuwa ameongozana na masheikh kadhaa akiwamo Amiri wa Shura ya Maimamu, Sheikh Musa Kundecha, alitoa tamko hilo katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana."Tunalaani kitendo alichofanyiwa Sheikh Ponda, tukio la kupigwa risasi na baadaye kudhalilishwa kwa kuondolewa hospitali wakati akipatiwa matibabu, ni jambo baya linakwenda kinyume na haki za binadamu.

"Tukio hili limeibua hisia kali kwa Waislamu, hivyo tunaitaka Serikali kuacha kuwatesa na kuwadhalilisha viongozi wa dini ya kiislamu, kwani kufanya hivyo ni kupandikiza chuki miongoni mwa Waislamu."Waislamu wamekuwa wakiamini kwamba, ufumbuzi wa suala la amani ya kweli na ya kudumu ya nchi ni kuweza kushughulikia madai ya msingi ya Waislamu dhidi ya Serikali ambayo ndio chanzo cha madai ya kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda," alisema Sheikh Katimba wakati akisoma tamko hilo lililosainiwa na Sheikh Juma Said Ally.Waitisha mkutano wa dharura kesho.

Kutokana na suala hilo, jumuiya hiyo imeitisha mkutano wa hadhara utakaofanyika kesho katika viwanja vya Nurul Yakin vilivyopo Wilaya Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo tamko litatolewa juu ya mustakabali wa suala hilo.Katika tamko hilo, Sheikh Katimba alisema kuwa hatua hiyo inaweza kuzidisha chuki baina ya Waislamu na vyombo vya dola kwa madai kuwa vimekuwa vikiwakandamiza Waislamu.

"Kitendo cha kumpiga risasi Sheikh Ponda na kisha kumchukua kutoka hospitali na kumpeleka gerezani kwa kukiuka taratibu ni kinyume cha haki za binadamu."Matibabu ni haki mojawapo kwa binadamu yeyote hata kama kuna wanaomtuhumu. Tuhuma si sababu ya kukiuka taratibu, kuvunja sheria na hata kumtisha unayemtuhumu, kwani njia hiyo haiwezi kutatua bali inazidisha ukubwa wa tatizo."Tunalaani kwa mara nyingine kitendo cha Polisi na Usalama wa Taifa kutenda vitendo vinavyoashiria uonevu kwa viongozi wa dini ya Kiislamu, pia tunaitaka Serikali kutenda uadilifu kwa raia wake hata pale inapoamini kuwa raia hao wana makosa.Sheikh Basaleh aonya.

Kwa upande wake mjumbe wa Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Alli Basaleh alikemea vikali tukio la kupigwa kwa Sheikh Ponda na kusema kuwa jamii inapaswa kupinga vitendo vya watu kuteswa na kunyanyaswa vinavyofanywa na vyombo vya dola."Hii ni ishara ya huko tuendako kwa baadaye, nchi inaweza kuingia kwenye machafuko, ni wazi kabisa hata katika mataifa ambayo amani imevurugika hali ilianza kama hivi kama njia ya kupinga uonevu wa Serikali dhidi ya watu wake.

"Tuwe makini na hali hii hakuna taifa lolote linaloweza kuhubiri amani pasipo kuwa na umoja na masikilizano baina ya viongozi wa Serikali na watu wake," alisema Sheikh Basaleh.Polisi waranda misikitini. Hata hivyo wakati viongozi hao wakiendelea na mkutano na waandishi wa habari jana, Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi katika Msikiti wa Mtambani ambapo gari tatu zilikuwa zikiranda nje ya msikiti huo huku zikiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).MTANZANIA iliwashuhudia askari hao wakiwa katika gari aina ya Defender zenye namba za usajili PT 2118 na PT 2083, ambazo zilikuwa nje ya msikiti huo.Hata hivyo wakati askari wakiwa wanaranda katika eneo hilo la Msikiti, baadhi ya makundi ya Waislamu walikuwa wakigawa vipeperushi vilivyokuwa vimeandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ambavyo vilihoji.

"Kwa nini Serikali ya CCM imempiga risasi Sheikh Ponda?"Mbali na Msikiti wa Mtambani, askari pia walikuwa wametanda katika Msikiti wa Magomeni Kichangani, ambapo anatoka Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Kundecha.MTANZANIA ilifanikiwa kunasa kipeperushi kilichosomeka kwa maneno yafuatayo; "Kwa nini Serikali ya CCM imempiga risasi Sheikh Ponda, polisi waliotaka kumuua sasa wamemteka kutoka Muhimbili hadi Segerea akiwa bado mgonjwa."Hii imefanyika ili mfumo wa kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali chini ya Mkataba (MoU)," ilisomeka sehemu ya kipeperushi hicho.Alipopigwa mkoani Morogoro.

Agosti 10, mwaka huu akiwa mkoani Morogoro, Sheikh Ponda, alidaiwa kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni risasi, ambapo Agosti 15, mwaka huu Jeshi la Polisi nchini liliripoti kushikiliwa kwa askari anayedaiwa kufyatua risasi hiyo.Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la MTANZANIA Agosti 11, mwaka huu, Sheikh Ponda alisema polisi walidhamiria kumuua kwa makusudi ili wapoteze ushahidi. Huku akidai kuwa jeraha lake analodai limetokana na kupigwa risasi.Sheikh Ponda alieleza kuwa alipigwa risasi na polisi wakati akiwa kwenye gari na wenzake. " Nilimuona kwa macho yangu askari mmoja ambaye alikua amevaa sare akinilenga kwa mtutu wa bunduki," alisema Ponda.:chanzo mtanzania.
 
Tanunua kesho Mtanzania nisome.
iyo miandishi labda uwe na lenzi mbinuko iliyobinuka
 
Ponda azua hofu
• WAISLAMU KUKUTANA LEO KUTOA
MSIMAMO
na Mwandishi wetu
HOFU ya kutokea vurugu za kidini imeanza
kuyakumba baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es
Salaam baada ya sakata la kupigwa risasi Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh
Ponda Issa Ponda.
Juzi idadi kubwa ya askari polisi walikuwa
wakirandaranda nje ya misikiti baada ya kuwapo
taarifa za waumini wa Kiislamu kufanya
maandamano ya kutaka ukweli wa sakata la
kiongozi huyo uanikwe.
Hata hivyo maandamano hayo hayakufanyika na
ikatangazwa kuwa leo katika viwanja vya Nurul
Yakin wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam
kutafanyika mkutano mkubwa.
Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
nchini, Rajabu Katimba, alisema wanapinga
kupigwa risasi kiongozi wao, kusomewa
mashtaka akiwa hospitalini na kupelekwa
gerezani kabla hajapata ahueni.
Anasema katika mkutano huo watalizungumzia
suala hilo kwa mapana na watapata msimamo
wa pamoja juu ya kulishughulikia.
Tanzania Daima Jumapili liliwasiliana na Sheikh
Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Issa Simba,
juu ya mkutano huo ambapo alisema yeye si
msemaji wa Shura ya Maimamu.
Alisema Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zipo
kisheria, hivyo zina mipaka yake na zinafanya
mambo kulingana na taratibu zilizojiwekea.
Alisema yeye ana mamlaka ya kuzungumzia
masuala yanayohusu Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA).
Wakati sakata hilo likizidi kuwa tete, familia ya
Sheikh Ponda imesema inakusanya ushahidi wa
tukio la kupigwa risasi kwa kiongozi huyo na
itauweka hadharani ukikamilika.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili,
msemaji wa familia ya Sheikh Ponda, Is-haq
Rashid, alisema licha ya ndugu yake kuwa
gerezani, familia inaendelea kukusanya
ushahidi wa kilichotokea Morogoro na
watakapokamilisha watauweka hadharani.
Alisema miongoni mwa ushahidi
wanaoukusanya ni taarifa za daktari aliyemtibu
Sheikh Ponda kwa mara ya kwanza mkoani
Morogoro.
“Tumechoshwa na udhalilishaji aliofanyiwa
ndugu yetu, sasa tumeamua kuweka hadharani
ushahidi wa maovu yaliyofanywa na polisi,”
alisema.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa
sakata la Ponda hivi sasa linaipa wakati mgumu
serikali na Jeshi la Polisi ambalo awali
lilikanusha kumpiga risasi kiongozi huyo.
Inadaiwa serikali inahofia sakata hilo litakuza
tofauti za kidini zilizoanza kujitokeza hivi sasa
miongoni mwa jamii lakini pia kulipaka matope
Jeshi la Polisi.
Inaelezwa kukamatwa kwa askari anayedaiwa
kufyatua risasi katika msafara aliokuwemo
Sheikh Ponda kunalenga kutuliza hali ya mambo
iliyoonekana kuiendea vibaya serikali na
vyombo vyake.
Tanzania Daima Jumapili limeelezwa licha ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile, kukana jeshi hilo kuhusika katika tukio
hilo, serikali imeamua kulivalia njuga ili
kutuliza hasira za waumini wa kiongozi huyo wa
kidini.
Kauli ya kamanda huyo ilizidisha hasira
miongoni mwa wanaomuunga mkono Sheikh
Ponda, huku wakitaka Shilogile ajiuzulu kwa
kusema uongo. Tanzania Daima Jumapili
limedokezwa kuwa tayari msako wa kumtafuta
daktari aliyemtibu kwa mara ya kwanza kiongozi
huyo wa kidini umeanza.
Daktari huyo inadaiwa ndiye aliyeweka wazi
kuwa jeraha la Sheikh Ponda limetokana na
risasi, ingawa hadi sasa hospitali na jina la
daktari huyo havijawekwa wazi.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili,
Kamanda Shilogile alisema wanafanya jitihada
za kumjua daktari na hospitali aliyopatiwa
matibabu kwa mara ya kwanza Sheikh Ponda.
“Polisi hatuna taarifa sahihi ya wapi alikotibiwa
kiongozi huyo, tunafanya jitihada za kujua ni
wapi alikotibiwa, habari kuwa alitibiwa hospitali
fulani hapa Morogoro hazina ukweli,” alisema.
Tanzania Daima Jumapili lilitaka kujua kwanini
polisi wanamshikilia askari anayedaiwa kufyatua
risasi hewani katika harakati za kumkamata
Sheikh Ponda wakati walisema hawahusiki.
Kamanda Shilogile alikataa kulitolea ufafanuzi
jambo hilo kwa madai kuwa kuanzia sasa suala
la Ponda litakuwa likizungumzwa na Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi waliounda tume ya
kulichunguza.
 
Watu wengi wapenda haki tunalaani kitendo cha Sheikh kupigwa risasi na Polisi.

Ila ndugu zangu waislamu jaribuni kuepuka matamshi Kama;

"Hii imefanyika ili mfumo wa kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali chini ya Mkataba (MoU),"

Kauli Kama hii inapandikiza tu chuki za kidini Na kusababisha kukosa support kutoka kwa wakristo.
 
Nani kawazuia waislam kuanzisha mou?

Kikwete ametoa ruhusa na kuwakaribisha Ikulu wapeleke mou yao sasa tatizo lipo wapi jamani?
 
Watu wengi wapenda haki tunalaani kitendo cha Sheikh kupigwa risasi na Polisi.

Ila ndugu zangu waislamu jaribuni kuepuka matamshi Kama;

"Hii imefanyika ili mfumo wa kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali chini ya Mkataba (MoU),"

Kauli Kama hii inapandikiza tu chuki za kidini Na kusababisha kukosa support kutoka kwa wakristo.

Wanataka serikali ndio iwaanzishie. Kama mahakama ya kkadhi
 
Kwa nini Serikali ya CCM imempiga risasi Sheikh Ponda?
Naona chama fulani kimeuza vizuri propaganda zake hapo!

Lakini ni ukweli pia kuwa iliyofanya ni serikali ya CCM, hili halipngiki.
 
Ngoja tuone mwisho wake

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wanataka serikali ndio iwaanzishie. Kama mahakama ya kkadhi
mtani wangu vipi leo? kwangu poa, ila leo sina la kuchangia uwanja wako mkuu ! Nimebakia na majinii wawili je nikutumie?
Ok weekendi njema....Asali ya nyuki wadogo ilimfikia Ms.Smile ?
 
PONDA_85a5f.png

SAKATA la Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, limeendelea kuwa gumzo katika maeneo mbalimbali, huku matamko makali yakitolewa dhidi ya Serikali.Sakata hilo limeonekana kutikisa na kutawala vyombo vya habari, baada ya kiongozi huyo wa dini kudaiwa kupigwa risasi, kusomewa mashtaka kitandani na baadaye kupelekwa gerezani chini ya ulinzi mkali akitolewa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI).Suala hilo limeibua hisia nyingine baada ya masheikh jijini Dar es Salaam, kutoa tamko lenye mwelekeo wa kupinga udhalilishwaji wa kiongozi huyo na kuionya Serikali juu ya mwenendo huo.Mbali na masheikh kutoa tamko jana, Jeshi la Polisi kwa upande wake nalo liliimarisha ulinzi katika Msikiti wa Kichangani, uliopo Magomeni na ule wa Mtambani uliopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.hdg

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajab Katimba, alisema kitendo hicho ni kibaya kwani kinapandikiza chuki baina ya Waislamu na Serikali.Sheikh Katimba ambaye alikuwa ameongozana na masheikh kadhaa akiwamo Amiri wa Shura ya Maimamu, Sheikh Musa Kundecha, alitoa tamko hilo katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana."Tunalaani kitendo alichofanyiwa Sheikh Ponda, tukio la kupigwa risasi na baadaye kudhalilishwa kwa kuondolewa hospitali wakati akipatiwa matibabu, ni jambo baya linakwenda kinyume na haki za binadamu.

"Tukio hili limeibua hisia kali kwa Waislamu, hivyo tunaitaka Serikali kuacha kuwatesa na kuwadhalilisha viongozi wa dini ya kiislamu, kwani kufanya hivyo ni kupandikiza chuki miongoni mwa Waislamu."Waislamu wamekuwa wakiamini kwamba, ufumbuzi wa suala la amani ya kweli na ya kudumu ya nchi ni kuweza kushughulikia madai ya msingi ya Waislamu dhidi ya Serikali ambayo ndio chanzo cha madai ya kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda," alisema Sheikh Katimba wakati akisoma tamko hilo lililosainiwa na Sheikh Juma Said Ally.Waitisha mkutano wa dharura kesho.

Kutokana na suala hilo, jumuiya hiyo imeitisha mkutano wa hadhara utakaofanyika kesho katika viwanja vya Nurul Yakin vilivyopo Wilaya Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo tamko litatolewa juu ya mustakabali wa suala hilo.Katika tamko hilo, Sheikh Katimba alisema kuwa hatua hiyo inaweza kuzidisha chuki baina ya Waislamu na vyombo vya dola kwa madai kuwa vimekuwa vikiwakandamiza Waislamu.

"Kitendo cha kumpiga risasi Sheikh Ponda na kisha kumchukua kutoka hospitali na kumpeleka gerezani kwa kukiuka taratibu ni kinyume cha haki za binadamu."Matibabu ni haki mojawapo kwa binadamu yeyote hata kama kuna wanaomtuhumu. Tuhuma si sababu ya kukiuka taratibu, kuvunja sheria na hata kumtisha unayemtuhumu, kwani njia hiyo haiwezi kutatua bali inazidisha ukubwa wa tatizo."Tunalaani kwa mara nyingine kitendo cha Polisi na Usalama wa Taifa kutenda vitendo vinavyoashiria
uonevu kwa viongozi wa dini ya Kiislamu, pia tunaitaka Serikali kutenda uadilifu kwa raia wake hata pale inapoamini kuwa raia hao wana makosa.Sheikh Basaleh aonya.

Kwa upande wake mjumbe wa Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Alli Basaleh alikemea vikali tukio la kupigwa kwa Sheikh Ponda na kusema kuwa jamii inapaswa kupinga vitendo vya watu kuteswa na kunyanyaswa vinavyofanywa na vyombo vya dola."Hii ni ishara ya huko tuendako kwa baadaye, nchi inaweza kuingia kwenye machafuko, ni wazi kabisa hata katika mataifa ambayo amani imevurugika hali ilianza kama hivi kama njia ya kupinga uonevu wa Serikali dhidi ya watu wake.

"Tuwe makini na hali hii hakuna taifa lolote linaloweza kuhubiri amani pasipo kuwa na umoja na masikilizano baina ya viongozi wa Serikali na watu wake," alisema Sheikh Basaleh.Polisi waranda misikitini. Hata hivyo wakati viongozi hao wakiendelea na mkutano na waandishi wa habari jana, Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi katika Msikiti wa Mtambani ambapo gari tatu zilikuwa zikiranda nje ya msikiti huo huku zikiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).MTANZANIA iliwashuhudia askari hao wakiwa katika gari aina ya Defender zenye namba za usajili PT 2118 na PT 2083, ambazo zilikuwa nje ya msikiti huo.Hata hivyo wakati askari wakiwa wanaranda katika eneo hilo la Msikiti, baadhi ya makundi ya Waislamu walikuwa wakigawa vipeperushi vilivyokuwa vimeandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ambavyo vilihoji.

"Kwa nini Serikali ya CCM imempiga risasi Sheikh Ponda?"Mbali na Msikiti wa Mtambani, askari pia walikuwa wametanda katika Msikiti wa Magomeni Kichangani, ambapo anatoka Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Kundecha.MTANZANIA ilifanikiwa kunasa kipeperushi kilichosomeka kwa maneno yafuatayo; "Kwa nini Serikali ya CCM imempiga risasi Sheikh Ponda, polisi waliotaka kumuua sasa wamemteka kutoka Muhimbili hadi Segerea akiwa bado mgonjwa."Hii imefanyika ili
mfumo wa kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali chini ya Mkataba (MoU)," ilisomeka sehemu ya kipeperushi hicho.Alipopigwa mkoani Morogoro.

Agosti 10, mwaka huu akiwa mkoani Morogoro, Sheikh Ponda, alidaiwa kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni risasi, ambapo Agosti 15, mwaka huu Jeshi la Polisi nchini liliripoti kushikiliwa kwa askari anayedaiwa kufyatua risasi hiyo.Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la MTANZANIA Agosti 11, mwaka huu, Sheikh Ponda alisema polisi walidhamiria kumuua kwa makusudi ili wapoteze ushahidi. Huku akidai kuwa jeraha lake analodai limetokana na kupigwa risasi.Sheikh Ponda alieleza kuwa alipigwa risasi na polisi wakati akiwa kwenye gari na wenzake. " Nilimuona kwa macho yangu askari mmoja ambaye alikua amevaa sare akinilenga kwa mtutu wa bunduki," alisema Ponda.:chanzo mtanzania.

Kumbe hii ni mikakati ya Wakristu?!?! ... Jamani...Ndugu zanguni, wako mapadre waliouwawa, yako makanisa yaliyochomwa moto, kupigwa mabomu, pamoja na masheikh kumwagiwa tindikali! Sidhani kama Wakristu kwa upande wao walitoa kauli ya kuwashutumu waisilamu! Serikali na vyombo vyake ina namna ya kufanya kazi zake. Inawezekana ni askari au pia inawezekana si askari! Masheik waliomwagiwa tindikali walimwagiwa na askari? Sidhani kama wakristu wanafurahia raia yoyote yule hata mpagani kutendewa kinyume na haki za binadamu! So the same iwe kwa wote.
Tusilaumu au tusitengeneze utamaduni wa ushindani wa dini. Kama ni hasira kati ya uislamu na askari ama CCM ama serikali basi ielekezwe huko, tazama Misri, wanachoma makanisa kutoa hasira zao dhidi ya wanajeshi ambao asilimia kubwa ni waislamu wenzao, so hata hapa kwetu majeshi yetu si ya dini moja! Tuungane pamoja kulaani vitendo kama hivyo na sio kunyooshea vidole dini nyingine. Kumbuka...inaweza kuwa wala si askari waliohusika..Tafakari!
 
Damu ya Padre Mushi kule Zanzibar akienda Ibadani inaililia Zanzibar. Makanisa yaliyochomwa moto kwa chuki yanaililia Tanzania. Bado hawakusema mfumo wa kuwakandamiza Wakristo na kuwapendelea Waislam uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali . Haya maneno ya Chuki dhidi ya Wakristo mbona yanazidi. Huu UDINI tanzania mpaka lini.
 
Watu wengi wapenda haki tunalaani kitendo cha Sheikh kupigwa risasi na Polisi.

Ila ndugu zangu waislamu jaribuni kuepuka matamshi Kama;

"Hii imefanyika ili mfumo wa kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali chini ya Mkataba (MoU),"

Kauli Kama hii inapandikiza tu chuki za kidini Na kusababisha kukosa support kutoka kwa wakristo.

Kushauri waislam waache kuongea nisawa na kusema subiri nikuchome kisu lakini usipige kelele
mimi nilifikiri utaishauri serikali iunde tume ya kuchunguza haya maneno au malalamiko ya waislam ni ya kweli au propaganda
mimi nadhan ndio ungekuwa ni ushauri sahihi kuiambia serikali iyapokee malalamiko halaf ichunguze lazima jibu lingepatikana
 
[MTANZANIA ilifanikiwa kunasa kipeperushi kilichosomeka kwa maneno yafuatayo; "Kwa nini Serikali ya CCM imempiga risasi Sheikh Ponda, polisi waliotaka kumuua sasa wamemteka kutoka Muhimbili hadi Segerea akiwa bado mgonjwa. "Hii imefanyika ili mfumo wa kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo uweze kudumu na kuweza kupewa fedha na Serikali chini ya Mkataba (MoU)," ilisomeka sehemu ya kipeperushi hicho.]

... Ni upuuzi mtupu!
"kamuulize mwenzenu MEMBE, ndg yake na JK aliyelelewa kwenye taasisi hizo na kupachikwa jina lisilo la dhehebu lake.
 
:disapointed:Kunya anye kuku akinya bata mavi yananuka.........vimewaka wakristo watuache.
 
[h=1]Wafuasi wa Ponda wapiga kambi Segerea[/h]
ico_plus.png
Share
ico_bookmark.png
[URL="javascript:CreateBookmarkLink()"]bookmark[/URL]
ico_print.png
Print
ico_email.png
Email
Email this article to a friend

Friend's Email Address
Your Email
Message

[TD="align: right"] Submit Cancel [/TD]

Rating

wafuasi.jpg
Sehemu ya wafuasi wa Sheikh Ponda Issa Ponda waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam jana ulioitishwa kulaani kukamatwa kwa kiongozi huyo. Picha na Michael Matemanga
 
Back
Top Bottom