Ponda agoma kwenda mahakamani

Ponda agoma kwenda mahakamani

Status
Not open for further replies.

Kakende

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2012
Posts
2,741
Reaction score
1,233
Morogoro na Dar. Kiongozi wa Taasisi ya Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana aligoma kufikishwa mahakamani kutoka mahabusu ya Gereza la Mkoa wa Morogoro, akidai kuchoshwa kuhairishwa kwa kesi yake kila anapofikishwa mahakamani.

Pamoja na kuchelewa kufikishwa mahakamani, kesi yake iliahirishwa tena hadi Juni 10 baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo kusema kuwa jalada bado halijarudishwa kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili wa kiongozi huyo, Bathelomeo Tarimo alilalamikia hali hiyo na kutaka haki itendeke kwa mteja wake.

Akizungumza jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza alisema kuwa kukwama kwa faili la Sheikh Ponda ni kutokana na maombi namba 25 ya mwaka 2014 yanayosubiri kusikilizwa mahakamani hadi sasa.

Msajili alisema kuwa maombi ya Sheikh Ponda ya kutaka kuharakisha usomaji wa rufaa ili utolewe uamuzi na kesi hiyo kumalizika au kuendelea, yatasikilizwa na Jaji Lawrence Kaduri, Juni 16.

Kwa upande wake, Wakili Tarimo alidai kuahirishwa kwa kesi hiyo kunatokana na kucheleweshwa kusomwa kwa rufani yake namba 89 ya mwaka 2013 aliyowasilisha Mahakama Kuu Septemba 14 mwaka 2013.

Wakili Tarimo alidai kuwa, rufaa hiyo inahusu moja ya shtaka linalomkabili Sheikh Ponda lililotokana na uamuzi uliotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Alidai kuwa majalada yote yanayohusu kesi ya Sheikh Ponda yapo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lakini cha kushangaza kesi imekuwa ikiahirishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, jambo ambalo alidai kuwa limeanza kumtia wasiwasi mteja wake.

Upande wa Jamhuri unaowakilishwa na Wakili Sunday Hyera uliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi na kupanga tarehe nyingine ya kutajwa wakati jalada halisi la kesi hiyo lililoitishwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, likiendelea kusubiriwa kuletwa kortini.

Chanzo: Mwananchi
 
huyo wakili Tarimo hana akili,kwa kwenda kumtetea gaidi mahakamani!
 
Hiyo ni thahir kwamba hakuna ubaguzi katika dn yetu hiyo ni haki na ni dalili tosha ya uthamini wa binaadam
 
Sheikh wetu ALLAH akupe subra, hawatakuridhia mayahudi na manaswara mpaka ufate mila zao
 
Allah afanye wepes kunako ugumu. Na ampe subra kunako kukata tamaa. Allahu l wakiil
 
Cha moto atakiona na bado hiyo kesi itaisha 2020 ndio kwanza mbichi kabisaaa..
 
Hivi Ukitakiwa Ukatoe Ushaidi Wako Huo Mahakamani, Uko Tayari We Mgalatia!!?? We Wadhani Ugaidi Ni Suala Dogo Kihivyo?? La Kupayuka Tu Midomoni, Mitandaoni, Magazetini, Vijiweni, Makanisani, Vilabuni, Mabaa Na Maeneo Mnayokutana!! Sasa Ponda Kwa Mashitaka Gani Ambayo Yanayofanya Awekwe Rumande Siku Zote Bila Ya Dhamana!! Hata Hao Mabwabwa Wenzenu Wanashindwa Watamfungulia Shitaka Gani Ambalo Litaweza Kumfunga Jela!! Wanahangaika Tu!! Na Hao Wanaowatuma Kufanya Hivyo (Bakwata) Kwa Ufisadi Na Wizi Wao!! Alafu Nawashangaa Sanaa Ninyi Watu,! Mwajifanya Wapambanaji Wa Ufisadi, Wizi, Dhuruma, Matumizi Ya Mabovu Ya Madaraka!! Leo Bakwata Wanafanya Hivyo Kwa Mali Za Waislam Na Uislam Wao!! Wanatokea Watu Thabiti Wa Kupinga Na Kupambana Nalo!! Wanambambikwa Makesi! Kama Akina Rwakatare, Godbless Lema Na Wengineo!! Ila Kwa Waislam (Sheikh Ponda) Mnawaita Magaidi!!! Je, Na Wale Boko Haram Tutawaita Vipi?? Acheni Chuki Zenu Kwa Waislam Na Uislam Wao!! Au Kama Hamuwezi, Basi Jaribuni Kujificha Kidogo!!! Leo Sheikh Ponda Akifungwa Jela! Ninyi Kama Kanisa (Chadema) Amtakuwa Mwatapata Faida Gani Hasa!!! Nilikuwa Nawaheshimu Sanaa!! Ila Now Days No!!! Watu Wabaya Sanaa Ninyi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom