Pombe.

Pombe.

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,395
Reaction score
1,439
Hi guys leo tutazungumzia pombe. Kama ilivyoada kila kitu kina faida zake na hasara zake, tuangalie faida kwa leo. Japo me sio mnywaji wa hiyo kizaga ila ntaleta faida nnazozijua, nyingine mtaongezea, hasara zake nahisi mnazifahamu, kama vile unaweza ukarudi umelewa ukampa mkeo simu na kusema "dada save namba zako ntakutafuta" ikakuhatarishia ndoa na nyinginezo. Leo ngoja niwatetee kidogo tu.

1. Inaondoa Stress.
Mnywaji au mlevi anakuwa na amani ya mda mfupi, hakumbuki matatizo aliyonayo.

2. Inaongeza kujiamini
Mnywaji au mlevi anakuwa anajiamini anaweza kila kitu kipindi ambacho yuko tungi.

3. Inasogeza choo karibu
Mywaji au mlevi ahangaiki kwenda chooni, choo kipo karibu sana, yani mlangoni.

4. Inafanya uso uwe soft.
Mnywaji au mlevi uso unakuwa soft, kulingana na kiwango kikubwa cha maji anayoyanywa, na ngano iliyotumika kutengenezea inategemea na nini anakunywa na je anakula chakula kizuri? Angalizo ni risk kwani mtu idadi ya aliyokunywa ni mapipa kadhaa ya pombe anaweza akapata kisukari mbeleni.

5. Inaongeza umakini
Akitaka kuvuka barabara anaangalia kushoto na kulia kama kuna gari kisha anaangalia juu kama kuna ndege then anavuka akitembea kwa mwendo wa zigzag kukwepa risasi.

Mwisho kabisa hasara za pombe ni nyingi kuliko faida.

 
Back
Top Bottom