Pombe za Bure kwa Wanaojitolea damu

Glucky

Senior Member
Joined
Dec 16, 2009
Messages
124
Likes
23
Points
35

Glucky

Senior Member
Joined Dec 16, 2009
124 23 35
Pombe za Bure Kwa Wanaojitolea Damu
3919626.jpg

Wednesday, January 13, 2010 5:22 PM
Benki moja ya damu ya Marekani imeanzisha kampeni ya 'Toa Damu Pata Bia' ambapo watu wanaojitolea damu watapewa pombe za bure ili kuwavutia watu wengi zaidi wajitolee kuchangia damu. Benki moja ya damu ya nchini Marekani iliyopo Tacoma, Washington imeanzisha kampeni ya kugawa pombe za bure kwa watu wanaojitolea damu katika vituo vyao.

Wachangia damu ambao hutakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 21, hupewa kuponi za lita moja ya pombe za bure.

Kampeni hiyo ambayo inakwenda kwa jina la "Toa Damu, Pata Bia" imewavutia watu wengi kiasi cha kwamba benki hiyo ya damu ina mpango wa kuongeza vituo vingi zaidi.

Watu wanaopewa kuponi baada ya kutoa damu hujipatia vinywaji vyao toka kwenye migahawa na baa mbali mbali za mjini humo.

Ili kuwaepusha watu na madhara ya pombe baada ya kutoa damu, kuponi zinazotolewa huanza kutumika masaa manne baada ya mtu kujitolea damu yake.
 

Forum statistics

Threads 1,191,647
Members 451,726
Posts 27,716,446