Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,792
Pombe inasababisha watt wa vigogo kufanya kufuru kivipi mkuu..??
Pombe na vinywaji hivi vikali walio kwenye mamlaka wanajua uingizwaji wake nchini na wakati mwingine wanatoa vibali wenyewe kama sio kumiliki biashara kabisa na kuchangia mapato....unadhani mkurugenzi wa say TBS akiongezewa mshahara kwa makusanyo bora bila kujali baadhi yanatoka kwenye bidhaa hatarishi watoto wake hawanufaiki? Si ni hawa hawa vijana wanatuharibia binti zetu kwenye night clubs? Si ni hawa hawa hawana heshima bara barani?
Mtu kama umezoea kufanya anasa hata ukiwa sio mnywaji utafanya anasa kwa style nyingine..hao watt wa vigogo wanaowaharibu Binti zenu nightclubs na kuvunja sheria barabarani hayo ndo maisha/tabia zao..sidhani kama kunywa pombe ndo kunawafanya hivyo..wangapi wanakunywa na hawazingui
Mkuu fikra nyepesi kama hizi zinauridhisha ubongo wako na kushindwa kufikiria matatizo makubwa yanayorudisha maendeleo ya taifa nyuma
basi tutakuwa hatukuelewana..mi nilikujibu vile ili kubaki kwenye mada husika..mana swali langu lilikuwa "pombe inasababisha vipi watt wa vigogo kufanya kufuru?" katika majibu yako nikaona umeongelea nightclubs na uvunjaji wa sheria nikajua ndo kufuru unazoziongelea ndo mana nikakujibu vile..Sina hakika kama ulinielewa....sijasema wanakunywa pombe...ila vipato vya wazazi wao ambao ndio walitakiwa kudhibiti ubora wa bidhaa ndiyo vinawavimbisha vichwa!
duuhh!! basi sawa mkuuHahahahaha! katika mambo hayo yanayochangia umasikini pombe iko juu japo sio ya kwanza.
Licha ya kuwa maisha ni magumu, vijana wengi wa sasa nchini Tanzania ni watumiaji wakubwa wa pombe tena zile zilizo kali.
Nakutana na vijana wanadai kuwa pesa ni ngumu na wakati mwingine wanadiriki kukuomba ukidhani kuna cha maana wanafanya kumbe ni kwenda kununulia pombe.
Hali hii ilizoeleka kuwa ni vijana wa mitaani walioshindwa kwenda shule ndio wanajihusisha na matumizi ya pombe kumbe upepo umebadilika na sasa hata wasomi wa vyuo vikuu wamekuwa ni watumiaji wa vileo.
Nimefanya uchunguzi usio na shaka na kubaini kuwa vijana wengi wa sasa wanaotumia vileo ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 17 kwenda juu na wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu.
Kwa vyovyote iwavyo hili ni tatizo ambalo linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya vijana na taifa la kesho.
Nadhani kuna watu wameliona na wanaliona hili, wewe kama mzazi/mlezi una mpango wa namna gani wa kumuepusha kijana wako asijiingize kwenye tabia mbovu ya unywaji wa pombe?
Tusemezane

Hahahahaha! katika mambo hayo yanayochangia umasikini pombe iko juu japo sio ya kwanza.