Pombe balaa.............

BIN BOR

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,013
407
Polisi walikuwa wanaranda kutafuta baa ambazo hazijafungwa saa sita usiku. Mara wakaiona baa moja ina wateja. Walipoingia pale, walevi karibu wote wakakimbia isipokuwa mmoja aliyelewa sana akaanguka chini kutoka kwenye stuli ndefu. Akawa kama kapoteza fahamu hivi. Polisi mmoja akamwagia maji na kumpepea yule mlevi akazinduka. Maongezi yakawa hivi......
Mlevi : Nini kinaendelea hapa?
Polisi : Ulianguka, ukapoteza fahamu. Sasa umezinduka amka twende kituoni.
Mlevi : Uliniona wakati naanguka?
Polisi : Ndio
Mlevi : Unanifahamu mimi?
Polisi : Hata! Sikufahamu.
Mlevi : Sasa afande, kama hunifahamu ulijuaje kuwa ni mimi ndiye niliyeanguka?
 
Dah! Hapo kinachofuata ni 'afande marwa hebu rifundishe hiri lirevi adabu!'
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom