Politics is an isssue of compromise and consensus! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Politics is an isssue of compromise and consensus!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Jun 3, 2011.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya! :pound:
  Kwa hali ilivyo na mambo yanavyokwenda, kuna dalili zinazoonyesha baadhi ya Wanamagambas wanaelekea kulazimika kufikia maamuzi magumu, lakini ya lazima na ya makusudi kama vile kuachana na chama ambacho kila kukicha kinawasakama kutokana na kelele zinazopigika huko mitaani! "Jiuzulu! Jiuzulu! Chama kimepoteza mvuto kwa ajili yako" (utadhani kilikuwa kinataka kuchumbiwa)!
  Msishangae siku za mbele wakaanza kudodosa uwezekano wa kukihama chama chao na kutafuta namna ya kujiunga na vyama vingine - huenda hata hiyo CDM! Wanaweza kupitia mlango wa nyuma au hata kwa kujionyesha kama waliotubu na kukiri kuwa mwee jamani, waligubikwa na giza la tamaa, hawakujua walitendalo, na sasa wanarejea kundini kwenye njia ya uzima na ukweli! Huku wakitokwa na machozi watawaelezeni namna wanavyojisikia hamu ya kuwa pamoja na walalahoi, wavuja jasho,na wananchi! Mwee! Kumbukeni kuna mifano mingi ya wanasiasa kulazimika kuwapokea hata waliokuwa wanatofautiana nao kwenye siasa inapofikia wakati wa kufanya maamuzi mazito kama vile ya uchaguzi. Tell me if this happens in Tanzania what should we expect? Aliyekuwa anaitwa fisadi ndio anakufuata wewe M-CDM kwa upoleee....chozi likimtoka......
  Kazi kwenu - maana, believe you me - hili linakuja! :dance:


   
Loading...