Polisi Yazuia Dhamana ya Eddy Riyami

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
JESHI la Polisi Visiwani Zanzibar limezuia dhamana ya mwanamkakati wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kutokana na tuhuma zinazomkabili.

Mwanamkakati huyo ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Mohammed Ahmed Sultan, maarufu Eddy Riyami, anatuhumiwa kutoa lugha ya matusi kwenye mitandao ya jamii.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Unguja jana, mmoja wa wanasheria wa Riyami ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema Jeshi la Polisi limezuia dhamana ya kiongozi huyo.
“Hadi sasa bado Jeshi la Polisi limeendelea kuzuia dhamana kwa Eddy Riyami, lakini mimi kwa kushirikiana na wanasheria wengine tunafanya jitihada suala hili lifikishwe mahakamani,” alisema mwanasheria huyo.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Salum Msangi, alisema wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo na watatoa taarifa zaidi kwa vyombo vya habari uchunguzi utakapokamilika.

Wakati hayo yakiendelea, CUF kimetoa taarifa kikisema hadi sasa hayajapatikana maelezo ya msingi kuhusu kinachoendelea kuhusu suala la Riyami.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Hamad Masoud Hamad, alisema hatua ya Jeshi la Polisi kuendelea kumshikilia mjumbe wa timu ya kampeni ya chama hicho, ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa siasa kwa wapinzani wa CCM.

Alisema kukamatwa kwa mjumbe huyo ni shinikizo linalofanywa na
baadhi ya viongozi wa siasa visiwani Zanzibar jambo ambalo si sahihi katika ujenzi wa demokrasia.
“Na jambo la ajabu zaidi hata mke wake alipokwenda makao makuu ya jeshi hilo hakuruhusiwa kuonana na mume wake jambo ambalo si la ustaarabu na utu.

“Ni vema sasa Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa utaalamu kama sheria na kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa,” alisema Masoud.
 
ccm ni waoga sana ! kama kweli anatuhumiwa kutukana , dhamana kwa ajili ya matusi tu nayo inakataliwa ?
 
Hizi nchi za afrika mashariki zinakoelekea zitaingia kwenye machafuko kama nchi za kiarabu.
 
Ujumbe upi aliandika.. wapi kwanza ha ha ha CCM oyee.. kidumu chama cha matatizo
 
KAMA Ni KWELI Anatuhumiwa Kwa Kutenda Kosa Hilo, Sasa Sheria Si INATAKA Mtuhumiwa Apelekwe Mahakamani Baada Ya Saa 24 Au 48 Baada Ya Kukamatwa!!! SASA Kumkamata Na Kumshikilia Tu, Dhamana Hakuna Na MAHAKAMANI Hapelekwi!!!! KWELI Sheria Ni Mapambo Tu Kwa Wanasiasa Wengi!!!! HATARI Vyombo Ambavyo Vinategemewa Kutenda Na Kusimamia Haki, Vikitumika Kisiasa Kwa Maslahi Yao!!!! Yale Yale Ya Sheikh Ponda, Miaka 2.3 Alizuiwa Mahabusu Kwa DPP KUZUIA DHAMANA, Mwisho Wake Kesi Za KUTENGENEZA, Ushaidi Hakuna, MAHAKAMA Imeshindwa Kumuhukumu, Akiachiwa Huru, Lkn Akiwa Na Kovu La RISASI Begani!!!! HAYO Ndio Maisha Ya VIONGOZI Wetu, Ambao Wanajitoa Ufahamu Kwa KUDHANI Wao Ni WATAWALA, Sio VIONGOZI!!!!
 
m

ahakama yake iko Yanganyika, na ataanzia kisutu, Vuteni subira ICC ya wazanzibari
Kwa Mujibu Wa KATIBA Ya ZANZIBAR Na Sheria Zao, Mtu Akitenda Kosa La Jinai Ktk Ardhi ya ZANZIBAR, Basi Atashitakiwa Ktk. Mahakama Za Zanzibar!! Sio Tanganyika!! LABDA Kwa MAHAKAMA KUU Ya Rufaa Tu!! NDIO Maana MAHAKAMA Ya KISUTU Wanashindwa Kusikiliza Kesi Ya Watuhumiwa Wa Ugaidi, Akina Sheikh FARID Na Wenzake!! IMEKUWA Nenda Rudi Tupu, Na Kuwaweka Tu Mahabusu Basi!!!!
 
Back
Top Bottom