Polisi yawagomea Lowassa, Sumaye, Mbowe Mwanza

Nitaingia kaburini bila kuipenda CCM na wanaccm yao mna roho mbaya kama mashetani
 
Familia acheni kumtesa marehemu mtajibu nini kwa mungu.mtu akifa azikwe .siasa ni mchezo mchafu
 
Lowasa akisindikizwa na waziri mkuu mstaafu mwenzie bwana Sumaye yuko jijini mwanza akisubiria taratibu za kumzika afisa wa chadema, pamoja na kuwepo ulinzi mkali inaonekana mji ni mtulivu, hakuna biashara ya kudeki barabara na hakuna mtu anaekesha akinywa pombe nje ya hotel aliyofikia. Karibu sana japo naimani hauli samaki kwa mila zenu basi hata supu ya mbuzi utakuwa unapata.
 
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!

Sisi sote ni watanzania na tunapaswa kuheshimiana. Wawache chadema wafanye mambo yao.

Tulishuhudia mwili wa mama yetu celina kombani ukiagwa na maelfu ya watanzania pale Dar na ukazikwa Morogoro.

Kama suala ni kipundupindu, hata wakati celina anaagwa kilikuwepo, pia watu walijaa kumzika Abdalah Kigoda huko Tanga. Au mikusanyiko ya baadhi ya viongozi ina kinga na ugonjwa huo?

Tunapaswa kuyakemea haya ili kuendelea kutunza amani ya nchi yetu.
 

Ulichokionesha ni wasiwasi wako kuliko uhalisia. Mambo ya Kudhania. Hebu eleza, Sheria gani inavunjwa na UKAWA kumuaga kiongozi mwenzao? Iwe mtaji kisiasa kwa nini na nyie maitafute mtaji kisiasa?
Ujinga wa Vyombo vya Dola na baadhi ya viongozi wa Serikali ndio unaowapa UKAWA umaarufu zaidi na zaidi mkidhani mnauondoa umaarufu wao. Wangeruhusiwa wakafanya yao kwa amani si wangekuwa wamemaliza? Ni kipi kinachoifanya Serikali ishindwe kujiamini kwenye mambo madogo hivyo?
Naanza kuona Rais Dr.Magufuli akihujumiwa kwa kuchafuliwa kwa Serikali yake Kukiuka Katiba aliyoapa Kuilinda iliyobeba ndani yake HAKI ZA BINADAMU.

Time will tell, hakuna aijuae kesho, kadiri wanavyokandamizwa ndivyo wanavyozidi kuwa Sugu na Wasioogopa!
 
Sifurahishwi kabisa na hicho kinachofanywa na polisi, ila ninapenda Sumaye na Lowassa waone kile kisu walichokuwa wananoa wakiwa madarakani kinakataje. Ni nadra sana kuona viongozi wa nchi hii wakiwa madarakani kukumea ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu na kuvunja katiba kunakofanywa na jeshi la polisi, Lowassa na Sumaye walipokuwa ccm pia waliamini na kushiriki aina hii ya utendaji wa jeshi la polisi na waliona sawa tu. Leo wanashangaa kwa ile saratani waliyoiachia kushika kasi. Na hili iwe fundisho kwa watawala wengine wote walioko madarakani leo, kwamba iwapo utaunga mkono tabia kama hizi za jeshi la polisi na ukakaa kimya usishangae huko mbeleni kimya chako kikakuponza kwa kufumbia macho tabia kama hizi. Angalizo muhimu, leo katiba inasiginwa lakini usishangae mambo yakabadilika na marais wetu wastaafu kushitakiwa. Mchezo huo unaanza kiutaniutani hivi hivi. Kama hamuamini angalieni kinachotokea Burundi kwa Nkurunzinza kalazimisha kurudi madarakani leo anatawala kwa mkono wa chuma huku akiwa hana amani kabisa na bado hatima yake haifahamiki. Yetu macho.
 
CDM wanatafuta umaarufu hadi misibani.

kama vipi wawachie ndugu wauchukue mwili wa mpendwa wao wakauzike kwani shida ipo wapi.
 
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!
HAMMY-D, ifikie wakati ubinadamu uwe zaidi ya siasa na maslahi yetu binafsi! Leo kuna msiba Dar es salaam wa katibu wa umoja wa wadreva. Niambie je! Dar hataagwa, na kama atazikwa kwao Mwanza, Mwanza hawatamuaga? Dar kipindupindu ndiko kimeanzia, Marehemu Kigoda,Kombani na Filikunjombe waliagwa tena kwa taratibu zetu za kiafrika kama ilivyo kawaida yetu. Hapa kafariki mtu wa CHADEMA mabomu yametanda, hivi napo hapa mnaongelea CHADEMA wanamatatizo? Ifikie wakati tuweke pembeni itikadi za vyama. Hivi mnataka ifikie wakati CCM akifariki azikwe na CCM na vyama vingine vivyo hivyo? Hii ni aibu, kama ndo mkuu wetu wa mkoa anaratibu hili kama inavyosemekana na wengi, basi mheshimiwa raisi hapa hana kiongozi. Kiongozi yeyote anaeonekana kutaka kuwagawa watanzania kwa jinsi yoyote na apingwe kwa nguvu zote! Hapa tumewaingiza ndugu zetu wa jeshi la polisi kwenye mgogoro usio wahusu hata kidogo! Hebu tusikie toka ofisi ya Afisa afya wa mkoa,Je! kipindupindu mkoani Mwanza kimefikai hatua ya kuzuia kuaga mwili wa marehemu alieuawa kwa mashoka na mapanga na si kwamba kafariki kwa kipindupindu? Kwa nini tamko hili lisitolewe na ofisi ya afisa afya wa mkoa? Nawapa pole sana polisi sababu wanajengewa chuki isiyowahusu. Mh raisi hesabu kwa Mwanza hauna kiongozi,unless kama hili lina baraka toka kwako kitu ambacho binafsi hakiingii akilini mwangu. Ninakufahamu na nmekufahamu siku nyingi.,hauko hivi labda ujifunze leo. Nakujua wewe si mwanza siasa bali ni mtu wa kazi. Wanasiasa watakuharibia nchi. Hapa kunajengwa chiki itakayozaa kuchukia serikali. Serikali iliyopita ilichukiwa kwa sababu ya kunyima watu haki zao.....tafadhari usijiingize kwenye huu upuuzi. Waachie waliozoea kunyanyasa wananchi kwa visingizo visivyokuwa na kichwa wala miguu. Hii double standard itaisha lini?
 
Nilikuwa nimeanza kumkubali Magufuli japo sikumpa kura yangu lakini kwa udhalimu huu unaofanywa na vyombo vya serikali anayoiongoza nitaendelea kuichukia ccm na wote wanaoiunga mkono.Naililia nchi yangu naona giza huko tuendako.

Inchi yako uchagani si kanda ya ziwa.
 

CHADOMO wanashangaza kweli!! ati wanajiuliza kama wao ni wahalifu?? hata kama sio wahalifu....inawezekana wameonyesha tabia za kihalifu hii inatosha kabisa kwa polisi kuchukua hatua!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…