Polisi yanasa Wasomali 46 wasio na vibali

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ZAIDI ya raia 46 wa Somalia, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuishi nchini bila ya kuwa na vibali.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo ya Temeke, Ilala na Kinondoni, wakiwa wamezagaa mitaani kinyemela, huku
akiwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Hussein Mgeni (34), Mohamed Abdi (23), Said Ally (23) na Jamali Mohamed (37).

Wengine ni pamoja na Faiza Ally (22), Nassoro Ahmed (34), Said Mrisho (33), Omary Abdi (32), Mohamed Ally (62), Abdallah Ismail (21), Kafil Kenan (20), Shahzad Tariq (22), Abdulal Shabaan (21, Abdu Adan (34), Range Ally (24) Adam Ibrahimu (27) pamoja na wenzao 30.

Aidha, Kova alisema Polisi inaendelea kufanya msako mkali dhidi ya wahamiaji wengine haramu ambao hawafuati utaratibu na sheria za uhamiaji ya nchi hii.

“Tunawaomba raia wema washirikiane na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi pindi wanapowaona au kumtilia shaka mtu yeyote ambaye hawamuelewi vizuri ili kufanikisha ukamataji wa watu wa namna hiyo,” alisema Kova.

Aidha, katika tukio jingine Kova alisema Polisi walifanya doria katika eneo la Mbezi kwa Msuguri na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wa ujambazi.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Yahaya Abdalla (24) mkazi wa Mbezi Makabe, George Steven (23) mkazi wa Mbezi, Kassim Yusuph (14), Mohamed Ibrahim (12) na Maulid Abdalla (16) na
kwamba wote wanaendelea kuhojiwa juu ya kuhusika kwao na matukio mbalimbali ya uhalifu.
 
Kova na wahamiaji halamu?!Uhamiaji wana fanya nini?na anauhakuka gani ni wahamiaji haramu wakati si fani yake;asilete ya mbia ya kudai pasipoti feki na watoaji waka sema halali;asiingilie Kazi zisizi muhusu;awashilikishe wenye Idara na ujuzi wa mambo ya wahamiaji
 
ZAIDI ya raia 46 wa Somalia, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuishi nchini bila ya kuwa na vibali.

..............


Wanaishi wengi btu bila vibali wapo tanga , arusha, na mikoa kibao au kuna shambulio fulani wamegundua hatuambiwi ili tusiwe na wasi wasi.

from age group I can smell somthing
 
Back
Top Bottom