Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Zingatieni sheria za br. ili kuepuka kufilisiwa kwa kulipa faini pindi mkamatwapo!
Lkn nina swali kwa wenye uelewa fedha hizi Polisi wanapeleka wapi? Yaani nini namtumizi yake?
Taarifa Za Usalama Barabarani Kanda Maalum
Oparesheni hiyo ililenga kutoa elimu kwa madereva na kuwakamata wale wanakaidi maelekezo yanayotolewa juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani na sheria za usalama barabarani.
Pia magari, pikipiki, na bajaji vilikaguliwa kujua uhalali wake wa kuwa barabarani. Makosa yaliyokamatwa ni pamoja na matumizi mabaya ya barabara, ulevi, kukatisha route, kutotii amri, ubovu wa magari na makosa mengineyo.
Katika oparesheni hiyo jumla ya magari na pikipiki zilizokamatwa ni 24,068 na kutozwa faini ya jumla TSHS 722,040,000/= (Millioni mia saba ishirini na mbili, arobaini elfu tu).
Aidha, lengo ya Jeshi la Polisi si kukusanya kiasi kikubwa cha fedha bali kuona watanzania wanazingatia na kutii sheria za usalama barabarani wakati wote wanapokuwa na vyombo vya moto.
S. N. SIRRO - DCP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM