Polisi yahaha kuficha waliovunjwa miguu wakiwa mahabusu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limekana kuwa kuna watu waliovunjwa miguu waliopo kwenye chumba cha watuhumiwa kilichopo kituoni na kusema anayetakiwa kusema kuwa kuna watuhumiwa waliovunjwa miguu au mikoni ni daktari, anaandika Josephat Isango.

Simon Sirro, Kamanda wa Polisi kanda maalumu ameliambia MwanaHALISI Online kuwa katika chumba cha watuhumiwa kituoni humo hana taarifa kama kuna watu waliovunjwa miguu na kama wapo jeshi la polisi huwa linawapeleka kwenye matibabu.

MwanaHALISI online lilitaka kupata ufafanuzi ikiwa hao watuhumiwa wanapata haki ya kupata matibabu na kwanini hawafikishwi mahakamani kwa kipindi kirefu vile kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza wajibu wa polisi kwa watuhumiwa.

Sirro alipoulizwa kuhusu baadhi ya watuhumiwa kukaa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani, alianza kuongea na simu nyingine na kukata ya mwandishi aliyekuwa na shauku ya kutaka kujua hatima ya hao watuhumiwa.

30 June mwaka huu akizungumza waandishi wa habari baada ya kuachiwa kwa dhamana, katika mahakama ya Kisutu, Tundu Lissu Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliwataka watetezi wa haki za binadamu na mawakili kupaza sauti ili haki za hao watanzania ziweze kutambuliwa.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) aliwataja Abdalah Bushiri, na Adnani Mohamed Mrutu kutoka Same ambao wamevunjwa miguu na wanateseka katika chumba hicho bila kufikishwa mahakamani au kupelekwa kwenye matibabu.

“La Pili ni juu ya wale niliowakuta kule shimoni, na nilioshinda nao usiku wa kuamkia leo, pale Central kuna watu wamekaa wengine wiki mbili, wengine wiki tatu, na wengine mwezi, kinyume na sheria ya Tanzania inavyoelekeza kuwa mtuhumiwa afikishwe mahakamani ndani ya saa 24, isipokuwa kama ni Jumamosi na Jumapili ambazo sio siku za kazi” alisema Lissu.

“Nilipokuwa ndani, nimeshuhudia mengi na kweli siku hiyo polisi walikuwa wanahaha, kamanda wa polisi ametutembelea zaidi ya mara 3 kwa usiku huo” alisisitiza Lissu.

Lissu alilala mahabusu ya polisi baada ya kuhojiwa na kunyimwa dhamana ambapo siku moja alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la uchochezi katika mahakama hiyo.

Kesi yake inasikilizwa na Hakimu Yohona Yongolo ambapo kwa upande wa mashitaka, unawakilishwa na Benard Kongolo, wakili wa serikali mkuu huku Lissu akitetewa na jopo la mawakili zaidi ya kumi wakiongozwa na Michael Ngalo akisaidiwa na Peter Kibatala.
 
JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limekana kuwa kuna watu waliovunjwa miguu waliopo kwenye chumba cha watuhumiwa kilichopo kituoni na kusema anayetakiwa kusema kuwa kuna watuhumiwa waliovunjwa miguu au mikoni ni daktari,

Kamanda yuko sahihi.Ndio maana hata mtu akifa unatakiwa kumpeleka hospitali daktari akathibitishe kama kafa kweli.Mtu huwezi ibuka tu kusema yule kavunjika mguu.Kuna watu wamepinda miguu unaweza dhani wamevunjika kumbe sio

Mfano ukiangalia macho ya Tundu Lisu ukasema ana makengeza utakuwa hujamtendea haki. Kisheria daktari ndiye anatakiwa aseme Tundu Lissu ANA MAKENGEZA hawezi ona mambo sawasawa na kuyaficha hayo makengeza inabidi awe anavaa miwani wakati wote.
 
JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limekana kuwa kuna watu waliovunjwa miguu waliopo kwenye chumba cha watuhumiwa kilichopo kituoni na kusema anayetakiwa kusema kuwa kuna watuhumiwa waliovunjwa miguu au mikoni ni daktari, anaandika Josephat Isango.

Simon Sirro, Kamanda wa Polisi kanda maalumu ameliambia MwanaHALISI Online kuwa katika chumba cha watuhumiwa kituoni humo hana taarifa kama kuna watu waliovunjwa miguu na kama wapo jeshi la polisi huwa linawapeleka kwenye matibabu.

MwanaHALISI online lilitaka kupata ufafanuzi ikiwa hao watuhumiwa wanapata haki ya kupata matibabu na kwanini hawafikishwi mahakamani kwa kipindi kirefu vile kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza wajibu wa polisi kwa watuhumiwa.

Sirro alipoulizwa kuhusu baadhi ya watuhumiwa kukaa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani, alianza kuongea na simu nyingine na kukata ya mwandishi aliyekuwa na shauku ya kutaka kujua hatima ya hao watuhumiwa.

30 June mwaka huu akizungumza waandishi wa habari baada ya kuachiwa kwa dhamana, katika mahakama ya Kisutu, Tundu Lissu Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliwataka watetezi wa haki za binadamu na mawakili kupaza sauti ili haki za hao watanzania ziweze kutambuliwa.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) aliwataja Abdalah Bushiri, na Adnani Mohamed Mrutu kutoka Same ambao wamevunjwa miguu na wanateseka katika chumba hicho bila kufikishwa mahakamani au kupelekwa kwenye matibabu.

“La Pili ni juu ya wale niliowakuta kule shimoni, na nilioshinda nao usiku wa kuamkia leo, pale Central kuna watu wamekaa wengine wiki mbili, wengine wiki tatu, na wengine mwezi, kinyume na sheria ya Tanzania inavyoelekeza kuwa mtuhumiwa afikishwe mahakamani ndani ya saa 24, isipokuwa kama ni Jumamosi na Jumapili ambazo sio siku za kazi” alisema Lissu.

“Nilipokuwa ndani, nimeshuhudia mengi na kweli siku hiyo polisi walikuwa wanahaha, kamanda wa polisi ametutembelea zaidi ya mara 3 kwa usiku huo” alisisitiza Lissu.

Lissu alilala mahabusu ya polisi baada ya kuhojiwa na kunyimwa dhamana ambapo siku moja alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la uchochezi katika mahakama hiyo.

Kesi yake inasikilizwa na Hakimu Yohona Yongolo ambapo kwa upande wa mashitaka, unawakilishwa na Benard Kongolo, wakili wa serikali mkuu huku Lissu akitetewa na jopo la mawakili zaidi ya kumi wakiongozwa na Michael Ngalo akisaidiwa na Peter Kibatala.
Kwani who is LISSU????mpka anachosema yeye tumuamini???? ili hali ALISHINDWA KUSIMAMIA maneno yake juu ya LOWASSA.....aaacheni kutafta kiki kwa maneno ya kumezeshwa KWANZA asimamie maaneno aliyoyasema JUU ya LOWASSAA ndio tuanze kumwamini kila asemacho sasa.....AFADHALI ya MNYIKA kasimamia MANENO YAKE
 
Lisu anataka haki za binadamu gani wakati wale jamaa wanajitokezaga kwa haki za chadema tu?
 
Kamanda yuko sahihi.Ndio maana hata mtu akifa unatakiwa kumpeleka hospitali daktari akathibitishe kama kafa kweli.Mtu huwezi ibuka tu kusema yule kavunjika mguu.Kuna watu wamepinda miguu unaweza dhani wamevunjika kumbe sio

Mfano ukiangalia macho ya Tundu Lisu ukasema ana makengeza utakuwa hujamtendea haki. Kisheria daktari ndiye anatakiwa aseme Tundu Lissu ANA MAKENGEZA hawezi ona mambo sawasawa na kuyaficha hayo makengeza inabidi awe anavaa miwani wakati wote.
Hayo ni ya mjini, mtu kafia kijijini .. lini apelekwe hospital kuthibitisha kifo?
 
Kamanda yuko sahihi.Ndio maana hata mtu akifa unatakiwa kumpeleka hospitali daktari akathibitishe kama kafa kweli.Mtu huwezi ibuka tu kusema yule kavunjika mguu.Kuna watu wamepinda miguu unaweza dhani wamevunjika kumbe sio

Mfano ukiangalia macho ya Tundu Lisu ukasema ana makengeza utakuwa hujamtendea haki. Kisheria daktari ndiye anatakiwa aseme Tundu Lissu ANA MAKENGEZA hawezi ona mambo sawasawa na kuyaficha hayo makengeza inabidi awe anavaa miwani wakati wote.
Wachaupunguani, mtu yuko mahabusu hapelekwi mahakamani wala hospitali huyo daktari atathibitisha vipi kama kavunjika na huku akiweseka maumivu. Omba yasikufike hayana mmoja
 
Kwani who is LISSU????mpka anachosema yeye tumuamini???? ili hali ALISHINDWA KUSIMAMIA maneno yake juu ya LOWASSA.....aaacheni kutafta kiki kwa maneno ya kumezeshwa KWANZA asimamie maaneno aliyoyasema JUU ya LOWASSAA ndio tuanze kumwamini kila asemacho sasa.....AFADHALI ya MNYIKA kasimamia MANENO YAKE
Wewe ni nani?????????
 
Wachaupunguani, mtu yuko mahabusu hapelekwi mahakamani wala hospitali huyo daktari atathibitisha vipi kama kavunjika na huku akiweseka maumivu.

polisi na magereza wana hospitali zao na madaktari wao au hujui hilo anaposema madaktari wathibitishe wepi?
 
Back
Top Bottom