Marco shija
Member
- Sep 20, 2015
- 64
- 36
Kuna suala la Polisi ambao wangekuwa wakifanya doria nyakati za usiku maeneo ya Kibaha kuanzia Maili Moja, picha ya Ndege na maeneo yake kwa Mbonde, kwa Matias, Mwendapole, kwa Mfipa, mpaka Kongowe huko wamekuwa kero kubwa sana isiwe kwa sisi madereva pikipiki tukiwa tunasubiri wateja wetu ambao ni abiria wanafika nyakati za usiku, wakikukamata wanatubeba kwenye magari yao na kutupeleka vituoni.
Wakifika huko wanatubandikishia mashtaka wanasema wametukuta na vitu vinavyosadikika ni vya wizi ikiwemo pikipiki zetu ambazo na sie tumepewa na watu tuendeshe vyombo vya moto ili kujipagia kipato chetu.
Sasa polisi nyie kwanini mnatuwekea makosa ambayo siyo ya kwetu? Ina maana Kibaha siku hizi ni eneo ambalo mheshimiwa Rais au mkuu wa mkoa amelitangaza kama lina hali ya tahadhari kama Kibiti?
Kwanini msiende Kibiti huko mkafanye haya? Na wanakamata siku za Ijumaa na Jumamosi ili ukifika kituoni unawaachia pesa kidogo wale na wao wanagawana.
Hivi wanajua no kwa jinsi ipi tunahangaika ili kuziwesesha familia zetu ziishi?
Polisi wa haya maeneo tumechoka na kero zenu hizi mkiendelea Kibiti inahamia huku. Fanyeni kazi ya kutulinda na siyo kutukamata na kutuwekea makosa yasiyotuhusu nyie ni watu ambao mnamafunzo ya kutosha ila kama mna mafunzo ya kubambikia makosa watu na sie tutawasaidia.