Polisi wekeni vituo vya ukaguzi wa magari

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,021
9,942
Kwa Sasa hivi kusafiri kwa gari binafsi ni adha kubwa trafik ni wengi na wanachouliza Ni kilekile. Kutoka Geita Hadi Mwanza Kuna vituo zaidi ya nane umbali usiozidi km 120.

Bado maeneo mengine ya nchi nadhani nusu ya polisi nchi hii ni trafik. Sasa hivi magari binafsi yanasafiri usiku Kati ya saa nne usiku Hadi saa 11 alfajiri kukwepa adha ya kupotezewa muda.

Napendekeza jeshi la polisi liweke vituo vya ukaguzi ukifika unapewa control namba unalipia gari inakaguliwa unapewa cheti kila unapokutana na trafik inaonyesha kupunguza muda wa kuulizana maswali yaleyale na kupotezeana muda barabarani.
 
Kusafiri usiku nayo ni risk, ukipata pancha halafu ni maporini huko utajutia sana, afadhali kupambana nao tu na ukiwa na chochote usiwe mchoyo

Sure Kuna sehemu zingine barabara nyembamba halafu unapata hitilafu mida mibovu aisee acha tuu.
 
mchana tatizo la Traffic ni mwendo zaidi ya 50km/h kwenye vibao vinavyokataza
zaidi ya hapo wakatalie
 
mchana tatizo la Traffic ni mwendo zaidi ya 50km/h kwenye vibao vinavyokataza
zaidi ya hapo wakatalie
Yaani wakikuona una gari jipya wanajua halina dosari anakuomba leseni akisha ichukua anakuacha anaendelea kusimamisha magari mengine utakaa hata nusu saa
 
Pili trafiki wanasababisha uharibifu wa barabara, unakuta wameweka kituo mahali ambapo hakuna sehemu ya kuegesha gari, so rami inabomoka.

Hii inahuzunisha sana.
 
Pili trafiki wanasababisha uharibifu wa barabara, unakuta wameweka kituo mahali ambapo hakuna sehemu ya kuegesha gari, so rami inabomoka.

Hii inahuzunisha sana.
Ni kweli wanasababisha uharibifu wa barabara, magari yanapochepuka, mie Kuna siku niliamua kusimama katikati ya barabara hakuniuliza kitu akaniambia niende
 
mchana tatizo la Traffic ni mwendo zaidi ya 50km/h kwenye vibao vinavyokataza
zaidi ya hapo wakatalie
 
Back
Top Bottom