figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Leo wanafunzi wa chuo cha sanaa Bagamoyo(TASUBA), wameamua Kuandamana kupinga Chuo cha sanaa Kuajiri Walimu wasio na sifa, na uundwaji wa kozi bila kufuata utaratibu kwa lengo la kujipatia fedha unaofanywa na uongozi wa Chuo hicho. Kumbuka hiki ndo chuo pekee cha sanaa Tanzania nzima.
Katika harakati za kuzuia maandamano hayo, Polisi wamewakamata baadhi ya Wanafunzi kadhaa akiwemo Msanii wa Muziki wa Asili, Vitali Maembe. wapo mikononi mwa polisi wilaya ya Bagamoyo kwa tuhuma za kuhusishwa na sakata la kitaaluma kwenye Chuo cha Sana'a Bagamoyo.
Maembe Vitali akidhibitiwa ipaswavyo
Katika harakati za kuzuia maandamano hayo, Polisi wamewakamata baadhi ya Wanafunzi kadhaa akiwemo Msanii wa Muziki wa Asili, Vitali Maembe. wapo mikononi mwa polisi wilaya ya Bagamoyo kwa tuhuma za kuhusishwa na sakata la kitaaluma kwenye Chuo cha Sana'a Bagamoyo.
Maembe Vitali akidhibitiwa ipaswavyo
Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio leo, Kamanda Mushongi amethibitisha kukamatwa na mwanamuziki huyo, na kwamba ameshafikishwa mahakamani, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kutotii amri ya polisi wakati wa maandamano ya wanafunzi katika chuo cha sanaa Bagamoyo.
“Kulikuwa kuna tatizo pale chuo cha sanaa Bagamoyo, kulikuwa kuna vurugu za wanachuo kwamba kukataa mitihani, wenyewe walikuwa wanataka kwamba chuo cha sanaa watoe mitihani ambayo iwe inatambulika na VETA, lakini wenyewe kama chuo wanasema wana mitihani yao, sasa kwa hiyo kuna vurugu za sintofahamu, ikabidi polisi iende pale, iliwakamata wanafunzi na kuwaleta kituo cha polisi.
Kamanda Mushongi aliendelea kuelezea ….............Yeye (Vitalis Maembe) alienda kule nasikia ana wanafunzi wake pale, akalazimisha kuingia ndani, kuitwa na polisi njoo utoke yeye hataki kutoka, tumeshampeleka mahakamani tu ndo dawa, hii mambo ya dhamana inasumbua”, alisema Kamanda Mushongi.
Pamoja na hayo Planet Bongo ilizungumza na Rose ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho, na kuelezea jinsi ilivyokuwa siku ya tukio.
Chanzo: EATV