Polisi watoa taarifa waliomua Shyrose Mabula

Polisi watoa taarifa waliomua Shyrose Mabula

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129

Mnamo Septemba 14, 2025 liliripotiwa tukio la kutekwa nyara kwa Shyrose Michael Mabula [21] aliyekuwa mwanachuo mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Mzumbe ndaki ya Mbeya Kitivo cha Sheria na watu wasiofahamika, ambapo Septemba 16, 2025 saa 5:00 usiku huko Mtaa wa Morovian uliopo Kata ya Isyesye Jijini Mbeya mwili wa mwanachuo huyo ulikutwa ukiwa umechomwa moto.

1759148891335.png

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza ufuatiliaji ili kuwabaini na kuwakamata waliohusika katika tukio hilo na Septemba 24, 2025 saa 4:00 asubuhi alikamatwa Marwa Nyahega John [25] mkazi wa Uzunguni “A” Mbeya ambaye katika mahojiano alikiri kuwa yeye pamoja na wenzake wawili ambao ni Edward Christopher Kayuni na Websta William Mwantebele kwa pamoja walikula njama na kumteka nyara Shyrose Michael Mabula [ambaye kwa sasa ni marehemu] kwa lengo la kujipatia fedha nyingi kutoka kwa baba yake mzazi aitwaye Dkt Mabula Michael.

Soma Pia: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, auawa Kikatili Baada ya Kutekwa

Baada ya kumteka walianza kupiga simu kwa familia yake kwa lengo la kujipatia fedha na iliposhindikana kupata fedha hizo kwa kuhofia kwamba watakamatwa walipanga kumuua binti huyo ili kupoteza ushahidi. Awali walimnywesha sumu ambayo ni dawa ya kuulia magugu mashambani aina ya “Round Up” iliposhindikana kuondoa uhai wake waliamua kumnyonga kwa kamba hadi kufa kisha kuuchoma moto mwili wake.

Baada ya kupata taarifa hiyo ufuatiliaji uliendelea na Septemba 25, 2025 alikamatwa mtuhumiwa Websta William Mwantebele [27] Mlinzi ambaye alikiri kushiriki kufanya tukio la utekaji na mauaji ya binti huyo na kueleza kuwa tukio hilo walifanya kwa kushirikiana na wenzake ambao ni Marwa Nyahega John na Edward Christopher Kayuni. Aidha alieleza kuwa anaweza kwenda kuwaonyesha Askari watuhumiwa wenzake kwani wamepanga kwenda mafichoni kwenye machimbo yaliyopo Wilayani Chunya.

Septemba 27, 2025 aliwapeleka Askari Polisi katika Kijiji cha Chalangwa eneo walilokuwa wamepanga kukutana. Askari Polisi waliweka mtego kwa ajili ya kumkamata mtu ambaye Websta William Mwantebele [Mtuhumiwa] atawaonyesha. Baada ya muda alifika mtu mmoja na mtuhumiwa huyo akawaeleza Askari kuwa huyo anayekuja ndiye Edward Christopher Kayuni waliyeshirikiana naye kumuua binti huyo.

1759224016941.jpeg
 
Vijana wameshapotea vifungo vinahusu , walidhani wamefikilia kwa kuitumia kichwa, kumbe wamefikilia kwa kuitumia mbwataa😃hao ni ndichi tu
 
Jamaa wapumbafu sana,wangepunguza dau wakachukua hela wakaendelea na maisha yao na kumuacha binti.

Wapate stahiki yao,sheria isiwafumbie macho.
 
Duuuhhh ila kuna watu wana roho ngumu.
Wamemuuwa kikatili sana.
Sumu kisha kumnyonga!!!
Huko Mbeya sijui kuna nini?
Jamaa katili wapo wengi.
Jamaa yetu wa kuitwa Cyril a.k.a Victor walimuuwa kwa kipigo cha nondo ya buchani kichwani. Wengi tu waliuwawa kwa kupigwa nondo 2005 - 2008 huko.
Miaka fulani ya 2000 walikuwa wanachuna ngozi watu!
Wanachafua sifa nzuri za mji wao wa Mbeya.
 
Wamemuuwa kikatili sana.
Sumu kisha kumnyonga!!!
Huko Mbeya sijui kuna nini?
Jamaa katili wapo wengi.
Jamaa yetu wa kuitwa Cyril a.k.a Victor walimuuwa kwa kipigo cha nondo ya buchani kichwani. Wengi tu waliuwawa kwa kupigwa nondo 2005 - 2008 huko.
Miaka fulani ya 2000 walikuwa wanachuna ngozi watu!
Wanachafua sifa nzuri za mji wao wa Mbeya.
Nahisi hii Mbeya kuwa na barabara kuu ya kuelekea Malawi na Zambia imefanya kuwa sana na mambo ya kiuhalifu. Vijana wengi wameharibikiwa na wengi ni kufuata mikumbo kujidai masela m*vi.
 
Siasa za hii nchi ndo zinafundisha vijana hizi tabia za kutekana na kuuana wakiamin kuna masrahi katika hivyo vitendo vya kikatili.
 
Mama Abdule asilete huruma hapa atie sign hawa kenge wanyongwe. "Justice should not only be done, but must also be seen to be done."
 
Kuna vitu vinatokea unaweza ukajiuliza ni kweli au upo ndotoni.
Shida ni umasikini au matatizo ya akili?
 
Naskia walibaka pia kabla ya kumuua.. au ni story za vijiweni.
 
Back
Top Bottom