kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 239
Unyama wa aina yake umetokea jana baada ya watu wenye silaha kali za kijadi kuvamia katika ofisi moja ya Serikali, kumtwaa mtu aliyekuwamo ndani na kumchinja kabla ya kumkata sehemu zake nyeti na kutimua nazo.
Alasiri ilipowasiliana kwa njia ya simu na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow, naye alikiri kuwapo kwa tukio hilo.
Kamanda Barlow akasema amemtuma kijijini hapo Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) wa Kiabakari na kwamba angetoa taarifa rasmi baada ya kupata taarifa kamili za tukio hilo.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu tuhuma za askari kukataa kwenda mapema kijijini hapo licha ya kuombwa msaada na uongozi wa Kijiji, Kamanda Barlow akasema kuwa Polisi wanapobaini kuwa usalama wao uko hatarini, kamwe hawawezi kwenda kwenye eneo la namna hiyo.
Mwandishi alipojaribu kutaka ufafanuzi zaidi, Kamanda Barlow akasema hawezi kufanya hivyo kwani bado hajapata taarifa kamili za tukio hilo.