Polisi: Wanne Kwa Mbaroni Kwa Kelele Dar

Polisi: Wanne Kwa Mbaroni Kwa Kelele Dar

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
33,783
Reaction score
40,564
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dare es Salaam limewakamata watu wanne na pikipiki zao, kwa tuhuma za kusababisha kero na fujo kwenye makazi ya watu kufuatia vyombo vyao vya moto ambavyo wanaviendesha kutoa kelele za milio mikali ya milipuko, suala ambalo ni kosa na kinyume cha Sheria ya Usalama Barabarani.

Jeshi hilo limewataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Masumbuko mkazi wa Tabata, Julius Dismas, mkazi wa Mwananyamala, Salehe Ally, mkazi wa Kijitonyama, Mohamed Rashid mkazi
wa Magomeni, ambao wote wapo mahabusu na hatua zaidi zinachukuliwa ili kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watumiaji wote wa barabara wakiwemo waendesha vyombo vya moto kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani pasipo kubugudhi watu wengine.

Screenshot 2026-03-06 205512.png
 
Hivi huyu mzee ndo ongea yake hivi.... Au ndo uzee
 
Back
Top Bottom