Polisi wanamkamataje mwizi wa simu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,293
Reaction score
2,620
Umeshawahi kujiuliza vipi polisi wanaweza kupata taarifa ya kichaa kilichoibiwa [emoji44].

Siku izi kesi zimekua nyingi za wizi wa simu Yani zimekua kha kesi za utapeli nyingi mnoo..!!

Uzi ni wako



Polisi wanapataje taarifa za Simu yako ikiwa umeibiwa au kupotea maana wapwa mnapenda kujuzwa...!!!!

Unapoenda kutoka taarifa ya kifaa chako kimeibiwa polisi watataka risiti uliyonunulia na taarifa za kifaa chako ukiwa huna basi jua utapigwa kalenda inshu yako mpaka ukome labda huwe uko vizuri zaidi.



Ikiwa Simu itaibiwa basi Kuna kitu kinaitwa IMEI number international mobile equipment identity. Ni namba za kipekee Katika Kila kifaa Cha Simu ambacho hakiwezi kufanana na kifaa chengine.



Polisi wao huchukua IMEI namba kisha wanaangalia kwenye database kupitia operator mbalimbali nchini ambao ni tigo voda, Airtel, halotel na nk.



Watoa huduma wa mitandao mbalimbali huweza kuwapa taarifa polisi kuhusu namba ya simu ya kifaa kilichoibiwa, SMS anazo chati na watu, location pamoja na call logs zake anazopiga au kupigiwa.



Yaani hata kama ukibadilisha line ukiweka nyingine uka format simu basi wao polisi kupitia IMEI namba wataweza kupata taarifa zako.

Polisi wao wanaangalia namba zako muhimu unazotumia kuwasiliana na watu Kisha wao wanaanza kuwasumbua ndugu jamaa au rafiki zako kwa namna yoyote ile mpaka wakupate pia ukiwa online wanajua eneo ulilopo basi wanakutimbia.



Polisi wao wanashirikiana na watoa huduma mbalimbali za Simu kuweza kupata taarifa za kifaa kilichopotea ndipo mtuhumiwa anadakwa kwa style hiyo.



Umeshawahi kuibiwa simu, hebu tuambie ulichukua hatua Gani kuipata ? Usisahau kushare kwa wengine wajifunze nasi.

Teknolojia ni Yetu sote

 
hawa jamaa wana app kabisa wanatumia ambayo wakiingiza tu imei ya simu husika znakuja taarifa zote za simu mpka calls,na kama data ikiwa on wanauwezo wa kuitrace mpka ilipo.

App ikishafeli sasa ndo wanatumia call logs kwa kuangalia watu ambao unawasiliana nao sana then wanamnyakua mmoja mpka akutaje ulipo
 
Kwa mfano hapa nilipo, watoa huduma wanaweza kujua IMEI yangu bila mimi kuwapa? Teknolojia ni Yetu sote
Naam kama simu yako umeweka line na inatumika kwenye database za wale watoa huduma wana uwezo wa kujua ip address yako IMEI namba pamoja na Mac address ya kifaa chako hata kama ujawatajia [emoji3577]
 
Naam kama simu yako umeweka line na inatumika kwenye database za wale watoa huduma wana uwezo wa kujua ip address yako IMEI namba pamoja na Mac address ya kifaa chako hata kama ujawatajia [emoji3577]
Eeeeh?? [emoji16]

Sasa kwa mfano mimi BICHWA KOMWEE, samia anaweza kunijuaa mimi ni nani na niko wapi kwa kutumia account yangu ya Jamiiforums? Au sijaelewa?

Au nijiandae tu kubinywa makende siku nikidabwa na samia, na venye huwa namuita MAUSHUNGI!

Ntabinywa makende hadi niombe poo.
 
Niliibiwa simu nikaenda polisi, sasa pale reception tukakutana polisi ambaye tunajuana. Baada ya kumwambia shida akanambia bwana braza kusema kweli simu UNAWEZA kuipata ila utatumia gharama kubwa kuliko bei ya simu ingawa kwa kuanzia utaambiwa utoe 50,000. Je unaendelea na process? Katika stori pale wakawa wanasema wanaokamatwa mara nyingi hawana uelewa na simu. Wajanja wanabadili imei au kuuza kimoja kimoja.
 
Simu huwa wanazipata kweli ila wanabaki nazo
 
Hata Moderator wa JF huwa wanaziona IP address zetu πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Lakini Maxence Melo ni Shujaaa sana na alishawahi kukutana na masaibu lakini hakutoa taarifa za Member wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…