Polisi wamvamia Bulaya hotelini

Polisi wamvamia Bulaya hotelini

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Easter-Bulaya-620x308.jpg


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya Chadema (UKAWA), Easter Bulaya akiwa jukwaani


Posted by:
Moses Mseti 8 hours ag



ASKARI Polisi zaidi ya 10 waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi, hivi karibuni walivamia hoteli aliyofikia mgombea ubunge wa jimbo la Bunda Mjini (Chadema) na kuanza kumpekua na watu wengine waliofika hotelini hapo. Anaandika Moses Mseti, Bunda … (endelea).



Tukio hilo lilitokea Septemba 9 saa 3:00 usiku wakati askari hao walipofika hatolini na kuanza upekuzi huku askari wengine wakiwa wameizingira hoteli hiyo waliokuwa na silaha (SMG) na mabomu ya machozi.



Hata hivyo katika tukio hilo ambako askari wengine walionekana wakiwa wamevalia sare polisi wengine kiraia wakiwa wamejaza mabomu ya machozi katika miili yao kitendo ambacho kilionesha kuwatisha na kuwakera wageni waliokuwa hotelini hapo.



Katika upekuzi huo uliofanyika hadi sa 4:30 usiku, askari hao hawakufanikiwa kumkamata mtu yeyote wala kusababisha uvunjifu wa usalama kwa mgeni na watu wengine waliokuwa nje karibu na hoteli hiyo.



Askari mmoja akizungumza na Mwanahalisi Online, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini alisema kufanyika kwa upekuzi huo kunatokana na kuwepo kwa taarifa kuna vijana waliohifadhi mapanga kwenye hotelini hapo.



Amesema licha ya kupata tarifa hizo za kuwepo na vijana wenye mapanga ambako hakutaja lengo la kuhifadhiwa kwake, alidai wamefanya upekuzi, chumba hadi chumba na hakuna walichoambulia.



“Kumbe taarifa tulizopewa ni za uongo na kuzushwa tuu mtaani, tunaomba samahani kwa usumbufu mlioupata, ni lazima ufanyike upekuzi kuweka usalama sawa,” alisema askari huyo.



Akizungumzia hali hiyo, Bulaya ambaye alifikia hoteli hiyo kwa lengo la kuendelea na mikutano yake ya kampeni, alidai kuwa askari hao kufanya upekuzi huo ni njama za CCM za kutaka kumkatisha tamaa na kwamba hawataweza.



Amesema wananchi wa Bunda wameishaichoka CCM na rangi zao na makopo yao (wagombea wao) hivyo ndiyo maana wanatumia mbinu hizo ili kuwakatisha tamaa na kamwe mbinu hizo hazitafanikiwa, kumrudisha nyuma katika harakati za kulikomboa Taifa.



Hata hivyo Bulaya hivi karibuni alichukuliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwenda kumhoji, mara baada ya kutoka amesema Mkuu wa Polisi Wilaya OCD, alionekana akipendelea upande mmoja wa CCM.



Bulaya ambaye anaoeneka kuungwa mkono na wananchi wa jimbo hilo hususani vijana na wanawake, amekuwa akimshambulia waziri wa Kilimo na Ushirika, Steven Wassira kwa kushindwa kuwatatulia kero zao, hiyo ndiyo inaelezwa kuwa chanzo za kufanyiwa fitina hizo.



Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kung`ombe na kuhudhuliwa na mamia ya wananchi, amesema Wassira ameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Bunda, ikiwemo tatizo la maji ambalo limekuwa `sugu` jimboni humo.



 
  • Thanks
Reactions: Yul
Ndio mwisho wa ujinga ujinga wao shem mwenyewe keshasepa kupata tafrija mamtoni sijui kwanini asihame tu kaz kututia hasara
 
si kuna taratibu za kisheria za kumfanyia mtu upekuzi? Huyu Bulaya hajui hizi taratibu? Je, wangekuja nayo kwa siri hayo mapanga na kuwabambikia? CCM wana visa vya kitoto hadi inakera. Huyu Wassira ndio mmoja wa think tank ya CCM
 
Je polisi wamemkamata huyo aliewapa taarifa za uwongo ? Je CDM nao wamejiandaa vipi kutoa taarifa za uongo ili wagombea wa CCM akiwemo Magufuli waweze kupekuliwa ? tumepewa taarifa za uongo !
 
chadema mpaka sasa amani ya wagombea iko ndogo imarisheni ulinzi zaidi
 
wasira atakoma mwaka huu,ni kumshughukia tarehe 25 october
 
Mwaka huu wataisoma namba A.K.A amekinaii watapigishwa kwata hadi wakome
 
Ile santuri ya ex-IGP Mahita kuwa CUF wameingiza makontena ya mapanga mbona imeshapitwa na wakati!! Hii ndiyo kazi Magufuli anajidaia kwenye majukwaa "Hapa Kazi Tu"?? This time watanzania hawadanganyiki.
 
Niraha sana walikwenda kwa uhakika utazani waliyaona yakohifadhiwa na badooo
 
Wasira ni mtu katili sana,mukataeni kwa kura, na maamuzi yake atakayoyachukua baada ya 25 oktb ya kung'ang'ania kinkurunziza
 
Hii nchi bhana chokochoko tu na maneno ndio tunaweza. . . .Wamepewa tip wameenda wamefanya ukaguzi hawakukuta kitu na wameomba radhi. . . . .

Mlitaka wakipewa taarifa wakae tu??!!
 
jamani ccm inapumulia kwa mshine mazishiyake ni octoba 25
 
Back
Top Bottom