Polisi wameanza kupiga tochi usiku

Polisi wameanza kupiga tochi usiku

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim aliliambia Mwananchi jana kuwa, wameanza kukagua magari nyakati za usiku baada ya kubaini madereva aliowataja kuwa ni wakorofi kuhamishia ‘vurugu’ za mwendo kasi usiku.
Alisema baadhi ya madereva huvunja sheria muda huo wakidhani Jeshi la Polisi halipo kazini.

“Tunakagua (magari) usiku na mchana na hao madereva wanaolalamika (kukamatwa usiku) tutawanyakua wakati wowote, mwendokasi wa mchana sasa hivi wameuhamishia usiku, kwa hiyo tutawakamata na kuwafungia leseni zao, haiwezekani ajali ziendelee kupoteza maisha ya watu kwa uzembe wa mtu mmoja,” alisema Muslim.

Alisema Novemba 30 walianza kuwakamata madereva wanaoendesha kwa kasi na kwamba, zaidi ya madereva 20 wameshanaswa kupitia tochi kati ya saa 4:00 usiku na kuendelea wilayani Same mkoani Kilimanjaro na Arusha.

Baadhi ya madereva waliozungumza na Mwananchi wamekilaumu Kikosi cha Usalama Barabarani kuwa kinafanya kazi zake kwa kuvizia.

Mmoja wa madereva hao, Shija Bujiku alisema alipigwa tochi saa nne usiku akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam kuandikiwa faini ya Sh30,000 kutokana na kosa la mwendo kasi.
 
Vile vibao aisee usiku hua havionekani vizur, tutapigwa wengi sana hizo tochi
 
Kama kibao cha hamsini kipo shuleni kwa sababu ya wanafunzi... Sasa usiku unampiga tochi hapo shuleni kwasababu gani? Jamani Polis sasa mnataka kuganyishwa kazi kama ROBOT
 
Mhhhh uwongo mweupe kabisa uhuu.... Mimi anipige toch nikiwa nipo 120 alafu akimbilie barabaran kama wanavyofanya mchana si nitawamwaga utumboooo.....
 
Sasa hawa madereva wa kubeba magazeti je?
 
Njia ya Moro dar nadhani zile tochi za kudumu zinafanya kazi. Walikula kichwa saa 5 usiku pale ubena. Kuna 50 ndefu na hizo tochi ni auto
 
mw sisimami asee.....nishawakimbia sengerama baada ya kuona wananipotezea mda wakati nawahi kivuko busisi.
 
Back
Top Bottom