Mkuu Mwiba nakubaliana nawe kwa kiasi fulani na post yako.Ila tu sikubaliani jinsi unavyo liunganisha suala lenyewe na siasa, hususan CCM.
Mimi si kwamba naitetea lakini sioni inavyoingia hapo moja kwa moja.
Suala la askari wale ni kukosa nidhamu, period.
Na inaelekea Kamanda Zelotte Steven ana suala la kujibu hapa.
Hawa jamaa mpakani hapo hawana supervision ya aina yoyote.
Kuonyesha askari hawa hapo mpakani ni sugu, niwaeleze kisa changu mwaka jana mwezi wa nane 2008.
Nilikuwa sijawahi kufika Ileje ingawaje naenda sana Mbeya ,Tukuyu.
Siku moja nikaamua kufika Ileje kwa njia ya kupitia KK,Chuo cha Magereza na kutokea njia panda Ilomba.
Sikujua hii ni njia ndefu sana maana ni milima mikali na sikujua Tanzania ni nzuri huko juu, maana you are literaly on top of the mountains.
Baada ya muda tulifika makao makuu ya Ileje ,Itumba,ambapo,tulikuta roadblock lakini hata hivyo hatukujali sana maana tulijua sisituko nchini mwetu hivyo tukashuka garini kupata soda baada ya mwendo mrefu.
Hapo ndio tukanote funny movements , akatumwa askari mmoja toka roadblock kutuchunguza kama ni watanzania au la na akaondoka.
Baada ya mapumziko kama ya dakika 10 tukaanza kuondoka, na pale roadblock sasa kukawa na askari kama wanne, wawili traffic na wawili kawaida mmoja sajenti, tukasimamishwa pale.
Kama kawaida wakaniuliza vielelezo vya gari (ambalo ni 4WD na brand new), nikawapa.Mmoja akaniamuru kutoka kwenye gari na kujaribu usukani kama wheel lock iko dis abled kwa kuhofia kuwa sisi niwezi tunaotoka S Africa na hivyo tunatumia panya routes kupeleka gari aidha Mbeya au Zambia au kwingineko.
Gari akaona liko ok na vielezo vyote vipo.Shida akasema gari bima imekwisha !!
Hii baada ya kuona ni sis ni wabongo halisi na si wageni.
Nikawahakikishia kwamba ni wenda wazimu tu kusafiri na gari mpya bila bima.Nikawa nimechokoza munkari.
Nikaamrishwa kupeleka gari kituoni, maana bima wameshindwa kuona vizuri.
Saahizo ni saa 10 nami naona mwendo nilioenda ni masaa karibu 5 hivyo ikabidi tuingie chemba.
Wakataka laki moja!!!
Nikawaambia kwa kosa lipi na lipi.
Mmoja akasema huyu mjuaji peleka gari kituoni na tumfungulie charge.
Sasa hapo ikabidi nitumie akili maana nikajua hawa wamezoea kuwa kamua watu huku na waliyokuwa wakifanya ni kweupee kwenye road block.
Tukabishana juu ya dau tukaishia kuwapa elfu 20 iliyoniuma sana.
Baada ya kukaa hapo karibu saa nzima wakaturuhusu, kabla ya kuondoka yule sajenti nikamwambia Bwana tutaonana tu si leo wala kesho tutaonana tu, Daslam wanakuja watu wengi tu pale kwa uhamisho, Hata Kamanda Kova kahamia hapo.
Jamaa akaniuliza jina nikampa nami nikamuuliza la kwake, kwanza akan'gaka lakini baadaye akaniambia.
Jina hilo nalifahamu sana.
Nikamwambia si fulani katika Idara fulani ya Serikali ni ndugu yako?
Sajenti akatweta.
Ee bwana nihifadhi mdogo wangu yule.
Nami kumhakikishia nikampigia simu ya mkononi ndugu yake tuakongea na nikampa Sajenti aongee naye.
Askari akatweta kweli kweli na kuomba radhi nami nikamuachia kwa kuwa kiendacho kwa mganga..
Somo nililopata hapo ni kuwa Askari kwenye vituo hivi vya mipakani pamoja na kupewa madaraka makubwa ya ulinzi wa nchi lakini wanatumia madaraka yao kwa kuendekeza ufisadi.
Haw wa kuingia Malawi sasa hiyo ni balaa tupu!
Kamanda Zelotte tupia macho hapo.