Polisi walikuwa wapi uwanja wa Taifa mpaka mashabiki wanaingia uwanjani na kung'oa nyasi bandia?

Kufuatia mvua kubwa na umeme kukatika uwanja wa Taifa wakati wa mechi kati ya Simba ya Tanzania na Al Misry kutoka Misri mechi ilisimama kwa muda lakini wakati huo huo baadhi ya mashabiki waliingia eneo la kuchezea mpira yaani pitch na kuanza kucheza kwenye maji yaliyojaa uwanjani na wengine kudiriki mpaka kung'oa majani yaliyowekwa juzi tu na Serikali.

Najiuliza tu mechi kama hizo huwa tuna walinda usalama wa kutosha pale uwanjani kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayevunja amani lakini niliona mpaka vijana wanaingia uwanjani na kuanza kung'oa majani hakuna polisi aliyekuwa karibu mpaka baada ya dakika kadhaa tena uharibifu umeshafanyika ndiyo polisi wanaingia uwanjani kuwatoa na kuwakamata baadhi yao.

Vyombo vya ulinzi iwe mvua iwe jua mnatakiwa kuwa alert muda wote, kwa jana pale ni hasara kwa Taifa kwasababu lazima marekebisho yafanyike tena kwa yale maeneo ambayo majani yameng'olewa.

Na wewe mtanzania unayeingia uwanjani kwa lengo la kung'oa majani hasa maana yake ni nini? Kwanini usilinde uwanja wako tena wa kimataifa.

Tuwe na tabia ya kulinda mali za nchi

Walkuwa busy na kupiga risasi hewani
 
Mkuu hiyo Aya ya mwisho katika maada yako ndio yenye maana!!
Huko juu kote ni makando tu!
Hivi polisi ni maroboti au binadamu kama wewe??
Hata kama kuwachukia, unadhan wao hawana damu? Mmmmh!!? Ila washenzi kwenye kupiga virungu hao nao!
 
Mkuu hiyo Aya ya mwisho katika maada yako ndio yenye maana!!
Huko juu kote ni makando tu!
Hivi polisi ni maroboti au binadamu kama wewe??
Hata kama kuwachukia, unadhan wao hawana damu? Mmmmh!!? Ila washenzi kwenye kupiga virungu hao nao!
OK
 
Back
Top Bottom