Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene amekiambia kituo cha Habari cha EATV kuwa, afya ya mbunge wa Bunda Mjini Ester Amos Bulaya, kuwa hali yake si nzuri akiwa mahabusu kwani presha yake imeshuka, na kwamba hajatoka tangu alivyopelekwa jana.
Jana Ester Bulaya alikamatwa na polisi kwa kosa la kuhudhuria mkutano wa mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, na mpaka sasa hajaachiliwa, huku mwenzake John Heche akitafutwa na polisi.
Wakati huo huo, Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mh. John Wegesa Heche, anatafutwa na jeshi la polisi mkoani humo, kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi mpaka sasa.
Tumaini Makene, amesema John Heche ametakiwa kufika polisi leo hii jioni.

"Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."