Mkuu Mlyafinono,
Kila nikikuona nakumbuka ulivyoniliza...
Kisheria mtuhumiwa akikiri kosa kwa kufanya confession mbele ya mlinzi wa amani, then hakuna ushahidi wowote unaohitajika hivyo mahakama haitahitaji kuita shahidi yoyote!.
Kama ni hivyo, na ni kweli mtuhumiwa huyo amekiri kosa, mambo yafuatayo yatafanyika.
- Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la mauaji na hatatakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji (jurisdiction). Kesi za mauaji husikilizwa na mahakama kuu!.
- Kama polisi watathibitisha wamekamilisha uchunguzi, then jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa DPP na hatimaye litahamishiwa mahakama kuu kupangiwa siku ya kusikilizwa by that time, kesi itakuwa imeishabadilishwa kutoka kesi ya mauaji (murder) hadi kesi ya kuua bila kukusudia (manslaughter)
- Kwenye ile confession, polisi wameshakaa na mwenzao na kumfundisha namna bora kabisa ya kukiri kosa ni kusema kuwa kutokana na vurugu na purukushani, bomu lilifyatuka kwa bahati mbaya na kumlipua marehemu!. Ili jinai ya mader itendeke, lazima kuwepo tendo la mauaji (actus reus) na nia ya mauaji (mens rea). Kwa vile jinai ya kifo imetokea hivyo actus reus imefanyika lakini kwa vile silaha ile ni bomu la machozi na sio ya risasi za moto, kazi ya bomu la machozi sio kuua, mahakama itakubali moja kwa moja kuwa mens rea ya kuua haikuwepo!.
- Siku ikifika, kesi hiyo itatajwa na kusikilizwa kwa siku moja tuu, ambapo mshitakiwa atasomewa kesi yake na mahakama itamuuliza kama analo la kujibu, wakili wake ataieleza mahakama kuwa mshtakiwa amekiri kosa, mahakama itathibitisha kwa kumsikiliza na kumsikiliza, kama hata kanusha kukiri kosa, then kesi hiyo itafungwa kwa kusikiliza final submission za mawakili wa pande zote, kisha mshtakiwa atapewa fursa ya kujitetea na kesi itakamilishwa na kupangiwa siku ya hukumu.
- Kwa vile hii ni public interest case, siku ya hukumu, mahakama itatoa adhabu kali ya zuga tuu ili kutuliza hasira za Watanzania ila mtuhumiwa hatatumikia adhabu hiyo!. Ila kisheria, maadamu hakuna mens rea, mshitakiwa angepaswa kuhukumiwa kwa adhabu ndogo tuu ya negligence kwenye matumizi ya silaha hivyo kusababisha kifo!. Kifo hicho kitahesabika kama kifo cha ajali kazini na kesi itakwisha.
- Akisha hukumiwa biashara ya kiserikali na jinai inakuwa imeishia hapo, jamaa atapelekwa gerezani siku mbili tatu na kuachiwa huru na kutafutiwa kazi nyingine ya kawaida na kendesha maisha yake ila sio eneo lile tena asije tambulika!.
- Familia ya marehemu wana uwezo wa kufungua kesi ya madai dhidi ya serikali kwa kifo cha mpendwa wao na serikali italipa fidia nono fasta fasta kupooza hasira za familia.
- Kihalisia, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa usalama wa taifa na IGP walipaswa kujiuzulu kama ile kesi ya mauaji Mwanza, waziri wa mambo ya ndani Ali Hasaan Mwinyi na Waziri wa usalama Peter Siyovelwa na igp, Saimon Pundugu walijiuzulu!.
- RPC, RSO, OCD na DSO, walipaswa wote kuunganishwa kwenye kesi hiyo lakini polisi wametumia ujanja kumshauri mmoja tuu ajitolee kuwa mbuzi wa kafara ila wengine wote waokoke japo this time, hawatafanikiwa kirahisi kama wanavyodhani!.
- All and all, damu ya Daudi Mwangosi haikumwagika bure, things will never be same again kwa polisi kutumia nguvu kubwa kuliko inayohitajika katika maandamano yoyote na hili limethibitishwa na maandamano ya Waislamu yaliyofuatia kifo hiki!.
Pasco.