Polisi wajiandaa kumnasua mwenzao anayetuhumiwa kumfyatulia bomu Daudi Mwangosi

Mkuu, je kama itathibitishwa kama bomu lililotumika lilikuwa ni la kivita? Funguka tena mkuu
huo ni utafiti wa maggid
Kwahiyo wewe ni chelea tu hata kama serikali inatumia mabomu ya kivita kwa wananchi wake?
 
Mkuu, je kama itathibitishwa kama bomu lililotumika lilikuwa ni la kivita? Funguka tena mkuu

Kwahiyo wewe ni chelea tu hata kama serikali inatumia mabomu ya kivita kwa wananchi wake?

inasemekana ni bomu la machozi lililopigwa (kwa kumlenga) at close range (<5m), tambua ngozi ya tumbo ni laini sana kuitoboa (hata kwa jiwe la kurusha unaweza) na tumboni kuna pressure kubwa.. na ndio maana matumbo huwa yanafuka nje kama povu. Hizo sumu za bomu la kivita umelishwa na gazeti la maggid 'kwanza jamii'
 
Tuko pamoja:
kinyume na hapo tofauti itakayojitokeza katika ''case proceedings'' itakuwa ni ndogo sana.

Sikubaliani na kukosekana intention ya kuua (actus rea) kwa sababu zifuatazo:

1. Silaha ililengwa kwa marehem, picha zinaonyesha
2. Hilo sio bomu'la machozi; tear gas cannister (kopo) halilipuki bali hufunguka baada ya internal chemical reaction likidondoka na kumwanga moshi wenye sumu ili macho yatoe machozi. Je kulikuwa na moshi wa kuwasha macho baada ya mlipuko hapo? Tangu lini kopo la gas likachanachana mwili wa binadamu hv zaidi ya gruneti la kivita!

Bila shaka uchunguzi utabaini.

Maoni yangu!
 
inasemekana ni bomu la machozi lililopigwa (kwa kumlenga) at close range (<5m), tambua ngozi ya tumbo ni laini sana kuitoboa (hata kwa jiwe la kurusha unaweza) na tumboni kuna pressure kubwa.. na ndio maana matumbo huwa yanafuka nje kama povu. Hizo sumu za bomu la kivita umelishwa na gazeti la maggid 'kwanza jamii'

Labda wewe mgeni hapa JF. Hilo gazeti limetoka jana. Watu tunajadili bomu lililotumika takribani "wiki" sasa

Halafu pressure ya tumbo ingeuchomoza utumbo tu lakini ile picha ya marehemu inaonesha mwili wote ulikuwa vipande vipande. Kawadanganye watoto wa chekechea.

Halafu usijione uko salama. Hivi vyombo vya ulinzi huwa wanauana wenyewe kwa wenyewe,mfano Kombe
 
Ahsante mkuu, natumaini wewe utakuwa umeeleweka zaidi ya mimi

Pia nimeipenda hiyo ya MALICE AFORETHOUGHT picha inaonesha wazi kabisa
 
Labda wewe mgeni hapa JF. Hilo gazeti limetoka jana. Watu tunajadili bomu lililotumika takribani "wiki" sasa

Halafu pressure ya tumbo ingeuchomoza utumbo tu lakini ile picha ya marehemu inaonesha mwili wote ulikuwa vipande vipande. Kawadanganye watoto wa chekechea.

Halafu usijione uko salama. Hivi vyombo vya ulinzi huwa wanauana wenyewe kwa wenyewe,mfano Kombe

sawa mtaalam wa mabomu ya kivita
 
Mkuu Mlyafinono,
Kila nikikuona nakumbuka ulivyoniliza...
Kisheria mtuhumiwa akikiri kosa kwa kufanya confession mbele ya mlinzi wa amani, then hakuna ushahidi wowote unaohitajika hivyo mahakama haitahitaji kuita shahidi yoyote!.

Kama ni hivyo, na ni kweli mtuhumiwa huyo amekiri kosa, mambo yafuatayo yatafanyika.
  1. Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la mauaji na hatatakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji (jurisdiction). Kesi za mauaji husikilizwa na mahakama kuu!.
  2. Kama polisi watathibitisha wamekamilisha uchunguzi, then jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa DPP na hatimaye litahamishiwa mahakama kuu kupangiwa siku ya kusikilizwa by that time, kesi itakuwa imeishabadilishwa kutoka kesi ya mauaji (murder) hadi kesi ya kuua bila kukusudia (manslaughter)
  3. Kwenye ile confession, polisi wameshakaa na mwenzao na kumfundisha namna bora kabisa ya kukiri kosa ni kusema kuwa kutokana na vurugu na purukushani, bomu lilifyatuka kwa bahati mbaya na kumlipua marehemu!. Ili jinai ya mader itendeke, lazima kuwepo tendo la mauaji (actus reus) na nia ya mauaji (mens rea). Kwa vile jinai ya kifo imetokea hivyo actus reus imefanyika lakini kwa vile silaha ile ni bomu la machozi na sio ya risasi za moto, kazi ya bomu la machozi sio kuua, mahakama itakubali moja kwa moja kuwa mens rea ya kuua haikuwepo!.
  4. Siku ikifika, kesi hiyo itatajwa na kusikilizwa kwa siku moja tuu, ambapo mshitakiwa atasomewa kesi yake na mahakama itamuuliza kama analo la kujibu, wakili wake ataieleza mahakama kuwa mshtakiwa amekiri kosa, mahakama itathibitisha kwa kumsikiliza na kumsikiliza, kama hata kanusha kukiri kosa, then kesi hiyo itafungwa kwa kusikiliza final submission za mawakili wa pande zote, kisha mshtakiwa atapewa fursa ya kujitetea na kesi itakamilishwa na kupangiwa siku ya hukumu.
  5. Kwa vile hii ni public interest case, siku ya hukumu, mahakama itatoa adhabu kali ya zuga tuu ili kutuliza hasira za Watanzania ila mtuhumiwa hatatumikia adhabu hiyo!. Ila kisheria, maadamu hakuna mens rea, mshitakiwa angepaswa kuhukumiwa kwa adhabu ndogo tuu ya negligence kwenye matumizi ya silaha hivyo kusababisha kifo!. Kifo hicho kitahesabika kama kifo cha ajali kazini na kesi itakwisha.
  6. Akisha hukumiwa biashara ya kiserikali na jinai inakuwa imeishia hapo, jamaa atapelekwa gerezani siku mbili tatu na kuachiwa huru na kutafutiwa kazi nyingine ya kawaida na kendesha maisha yake ila sio eneo lile tena asije tambulika!.
  7. Familia ya marehemu wana uwezo wa kufungua kesi ya madai dhidi ya serikali kwa kifo cha mpendwa wao na serikali italipa fidia nono fasta fasta kupooza hasira za familia.
  8. Kihalisia, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa usalama wa taifa na IGP walipaswa kujiuzulu kama ile kesi ya mauaji Mwanza, waziri wa mambo ya ndani Ali Hasaan Mwinyi na Waziri wa usalama Peter Siyovelwa na igp, Saimon Pundugu walijiuzulu!.
  9. RPC, RSO, OCD na DSO, walipaswa wote kuunganishwa kwenye kesi hiyo lakini polisi wametumia ujanja kumshauri mmoja tuu ajitolee kuwa mbuzi wa kafara ila wengine wote waokoke japo this time, hawatafanikiwa kirahisi kama wanavyodhani!.
  10. All and all, damu ya Daudi Mwangosi haikumwagika bure, things will never be same again kwa polisi kutumia nguvu kubwa kuliko inayohitajika katika maandamano yoyote na hili limethibitishwa na maandamano ya Waislamu yaliyofuatia kifo hiki!.

Pasco.

Salute Mkuu Pasco! Kama ndo hivyo tunaomba picha zake ili tumhukumu kwa 'bahati mbaya'.
 
inasemekana ni bomu la machozi lililopigwa (kwa kumlenga) at close range (<5m), tambua ngozi ya tumbo ni laini sana kuitoboa (hata kwa jiwe la kurusha unaweza) na tumboni kuna pressure kubwa.. na ndio maana matumbo huwa yanafuka nje kama povu. Hizo sumu za bomu la kivita umelishwa na gazeti la maggid 'kwanza jamii'
Labda wewe mgeni hapa JF. Hilo gazeti limetoka jana. Watu tunajadili bomu lililotumika takribani "wiki" sasa

Halafu pressure ya tumbo ingeuchomoza utumbo tu lakini ile picha ya marehemu inaonesha mwili wote ulikuwa vipande vipande. Kawadanganye watoto wa chekechea.

Halafu usijione uko salama. Hivi vyombo vya ulinzi huwa wanauana wenyewe kwa wenyewe,mfano Kombe
Sikubaliani na kukosekana intention ya kuua (actus rea) kwa sababu zifuatazo:

1. Silaha ililengwa kwa marehem, picha zinaonyesha
2. Hilo sio bomu'la machozi; tear gas cannister (kopo) halilipuki bali hufunguka baada ya internal chemical reaction likidondoka na kumwanga moshi wenye sumu ili macho yatoe machozi. Je kulikuwa na moshi wa kuwasha macho baada ya mlipuko hapo? Tangu lini kopo la gas likachanachana mwili wa binadamu hv zaidi ya gruneti la kivita!

Bila shaka uchunguzi utabaini.

Maoni yangu!
sawa mtaalam wa mabomu ya kivita
Na huyo je?
 
Polisi wanaandaa mashitaka wakimshataki nani ,au umekusudia wanaandaa ushaidi ?
 
Sasa kwa case ya iringa nani atajitolea kuwa bangusilo??RPC!sidhani maana anajua atakosa mafao yake anastaafu karibuni sana...nadhani june mwakani!!hawezi kubali kujitoa mhanga!!
 
Kuna taarifa kuwa polisi ambao wanaandaa mashitaka kuhusu kijana mwenzao anyetuhumiwa kwa mauaji ya Daudi Mwangosi wanapanga mbinu za kumnasua kijana huyo kwa kutopeleka mashahidi mhakamani baada ya kufunguliwa kwa kesi hiyo.

Wanasheria mtusaidie hii imekaaje kisheria?

Mkuu nashukuru kuona umerudi tena. Maana kuna ku-upepo fulani kalivuma hapa JF juu yako baada ya tukio la kuuwawa kwa Mwangosi (RIP).
 
Back
Top Bottom