Polisi wajiandaa kumnasua mwenzao anayetuhumiwa kumfyatulia bomu Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wajiandaa kumnasua mwenzao anayetuhumiwa kumfyatulia bomu Daudi Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlyafinono, Sep 10, 2012.

 1. M

  Mlyafinono Senior Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kuwa polisi ambao wanaandaa mashitaka kuhusu kijana mwenzao anyetuhumiwa kwa mauaji ya Daudi Mwangosi wanapanga mbinu za kumnasua kijana huyo kwa kutopeleka mashahidi mhakamani baada ya kufunguliwa kwa kesi hiyo.

  Wanasheria mtusaidie hii imekaaje kisheria?
   
 2. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Ni sawa na kwenda kulewa wakati una matatizo yanayokukabili, pombe ikiisha matatizo yapo palepale. Wanaficha lakini kurudisha Imani kwa wananchi lazima mambo yote yafanywe kwa uwazi
   
 3. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wala hakuna haja ya kushughulika nao. Wawakomalie wakubwa zao waliowatuma kufanya huo ufedhuli. Damu ya mtu huwa haiendi bure.
   
 4. commited

  commited JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mkuu Mungu wetu ni mwaminifu sana hayatapita hivihivi haya mambo ya hawa wauaji... Kuna jambo litafanyika... ni nani anayaweza kushindana na aliyemuumba? Acha tu walete ujanja wa mbuni wa kujificha mchangani wakati shingo na makalio vinaonekana.
   
 5. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Mungu si mvivu kama Mwigulu Nchemba .... atahukumu fairly
   
 6. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Idk, hii sioni kama imekaa vizuri, it sounded more defensive kana kwamba aliyeandika ni mmoja wa anaoandaa hizo mbinu so anatanguliza tule tudege ambatwo hatuna rubani kunusa -nusa...!!
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mtu ni mali ya JMT na sio polisi!
   
 8. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja
   
 9. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  N upepo utapita tu.
   
 10. t

  tenende JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bila kupiga kelele kwa nguvu ni rahisi mwizi wa kuku kunyongwa, kuliko muuaji aliyetumwa kuua na wakubwa!.. Kama hakutumwa nani kajiuzulu au kushinikizwa kujiuzulu baada ya tukio!.. Ona wakubwa wako kimyaaa! Utafikiri mauaji yamefanyika malawi!..
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mwanzisha thread jana naona kuna thread ilikuwa inakuhusu so sijui kama umewajibu thread........kumbe upo alive watu walishajuwa umeondoka kumbe sio wewe
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Hayo mashtaka dhidi yake yamefunguliwa na nani?
   
 13. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Thank you, Good questions !!
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :biggrin1::biggrin1:
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,277
  Trophy Points: 280
  bonge la signature
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mlyafinono,
  Kila nikikuona nakumbuka ulivyoniliza...
  Kisheria mtuhumiwa akikiri kosa kwa kufanya confession mbele ya mlinzi wa amani, then hakuna ushahidi wowote unaohitajika hivyo mahakama haitahitaji kuita shahidi yoyote!.

  Kama ni hivyo, na ni kweli mtuhumiwa huyo amekiri kosa, mambo yafuatayo yatafanyika.
  1. Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la mauaji na hatatakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji (jurisdiction). Kesi za mauaji husikilizwa na mahakama kuu!.
  2. Kama polisi watathibitisha wamekamilisha uchunguzi, then jalada la kesi hiyo litapelekwa kwa DPP na hatimaye litahamishiwa mahakama kuu kupangiwa siku ya kusikilizwa by that time, kesi itakuwa imeishabadilishwa kutoka kesi ya mauaji (murder) hadi kesi ya kuua bila kukusudia (manslaughter)
  3. Kwenye ile confession, polisi wameshakaa na mwenzao na kumfundisha namna bora kabisa ya kukiri kosa ni kusema kuwa kutokana na vurugu na purukushani, bomu lilifyatuka kwa bahati mbaya na kumlipua marehemu!. Ili jinai ya mader itendeke, lazima kuwepo tendo la mauaji (actus reus) na nia ya mauaji (mens rea). Kwa vile jinai ya kifo imetokea hivyo actus reus imefanyika lakini kwa vile silaha ile ni bomu la machozi na sio ya risasi za moto, kazi ya bomu la machozi sio kuua, mahakama itakubali moja kwa moja kuwa mens rea ya kuua haikuwepo!.
  4. Siku ikifika, kesi hiyo itatajwa na kusikilizwa kwa siku moja tuu, ambapo mshitakiwa atasomewa kesi yake na mahakama itamuuliza kama analo la kujibu, wakili wake ataieleza mahakama kuwa mshtakiwa amekiri kosa, mahakama itathibitisha kwa kumsikiliza na kumsikiliza, kama hata kanusha kukiri kosa, then kesi hiyo itafungwa kwa kusikiliza final submission za mawakili wa pande zote, kisha mshtakiwa atapewa fursa ya kujitetea na kesi itakamilishwa na kupangiwa siku ya hukumu.
  5. Kwa vile hii ni public interest case, siku ya hukumu, mahakama itatoa adhabu kali ya zuga tuu ili kutuliza hasira za Watanzania ila mtuhumiwa hatatumikia adhabu hiyo!. Ila kisheria, maadamu hakuna mens rea, mshitakiwa angepaswa kuhukumiwa kwa adhabu ndogo tuu ya negligence kwenye matumizi ya silaha hivyo kusababisha kifo!. Kifo hicho kitahesabika kama kifo cha ajali kazini na kesi itakwisha.
  6. Akisha hukumiwa biashara ya kiserikali na jinai inakuwa imeishia hapo, jamaa atapelekwa gerezani siku mbili tatu na kuachiwa huru na kutafutiwa kazi nyingine ya kawaida na kendesha maisha yake ila sio eneo lile tena asije tambulika!.
  7. Familia ya marehemu wana uwezo wa kufungua kesi ya madai dhidi ya serikali kwa kifo cha mpendwa wao na serikali italipa fidia nono fasta fasta kupooza hasira za familia.
  8. Kihalisia, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa usalama wa taifa na IGP walipaswa kujiuzulu kama ile kesi ya mauaji Mwanza, waziri wa mambo ya ndani Ali Hasaan Mwinyi na Waziri wa usalama Peter Siyovelwa na igp, Saimon Pundugu walijiuzulu!.
  9. RPC, RSO, OCD na DSO, walipaswa wote kuunganishwa kwenye kesi hiyo lakini polisi wametumia ujanja kumshauri mmoja tuu ajitolee kuwa mbuzi wa kafara ila wengine wote waokoke japo this time, hawatafanikiwa kirahisi kama wanavyodhani!.
  10. All and all, damu ya Daudi Mwangosi haikumwagika bure, things will never be same again kwa polisi kutumia nguvu kubwa kuliko inayohitajika katika maandamano yoyote na hili limethibitishwa na maandamano ya Waislamu yaliyofuatia kifo hiki!.

  Pasco.
   
 17. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja:
  kinyume na hapo tofauti itakayojitokeza katika ''case proceedings'' itakuwa ni ndogo sana.
   
 18. m

  mwakitundilo Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salute Mkuu Pasco!
   
 19. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu, mfano ile picha inayoonesha FFU wanawafyatulia mabomu watu wakiwa ndani ya nyumba! Kile kitendo ilitakiwa kiwe kimekemewa na Rais, IGP au waziri Nchimbi
   
 20. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu, je kama itathibitishwa kama bomu lililotumika lilikuwa ni la kivita? Funguka tena mkuu
   
Loading...