Polisi wajeruhi raia kwa kipigo Rungwe mkoani Mbeya

ngogo

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
359
54
Jeshi la Polisi Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya limewajeruhi raia kadhaa kwa kipigo na kuharibu mali zikiwemo nyumba za raia Wilayani hapa, Pamoja na kujeruhi na kuharibu mali za raia hao wa Mamlaka ya mji mdogo wa Busokelo katika Kata ya Luangwa na Kata ya Ikama pia Polisi hao walipora fedha, nguo na hata kula vyakula walivyovikuta tayari vimepikwa, Uharibifu huo ni Pamoja na kuvunja milango ya nyumba za raia, kuvunja majokofu,Tv, vitanda na vifaa vingine, hali hiyo ilisababisha shughuli za maendeleo kusimama kwa siku kadhaa kuanzia 29/09/2014 walipoanza kutembeza kichapo mpaka leo hii bado shughuli za kipigo zinaendelea, Katika kutekeleza jukumu lao la kupiga kama walivyoamuriwa na viongozi wao hawachagui wa kumpiga kuanzia watoto mpaka wazee, lakini pia hawakuishia hapo, bali kila siku wanawakamata wananchi wa maeneo hayo na kuwapeleka katika kituo cha Polisi Tukuyu, hali za majeruhi hao ni mbaya na hawana msaada wa kimatibabu kwani polisi wanawazuia kupata fomu namba tatu ya polisi (PF3) ili kuweza kupata matibabu kwa mujibu wa sheria, Viongozi wa polisi walipoulizwa wanasema waache wapigwe tu kwa kuwa wananchi wa maeneo hayo wana itikadi ya upinzani
 
Back
Top Bottom