Polisi wachunguza vitisho kwa vigogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wachunguza vitisho kwa vigogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Dec 5, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 05.12.2008 0006 EAT

  • Polisi wachunguza vitisho kwa vigogo

  *Ni Sitta, Mwakyembe, Kilango na Mengi
  *Spika: Huu ni uhalifu wa kisiasa, sitishiki

  Na Waandishi Wetu
  Majira

  JESHI la Polisi nchini linafanya upelelezi wa kuwepo madai ya kutishiwa maisha baadhi ya viongozi na wanahabari mashuhuri nchini katika kile kinachoonekana kuwa ni mfululizo wa watu wanaokemea ufisadi nchini kuandamwa, umebaini uchunguzi wa Majira.

  Viongozi walioko katika orodha ambayo imelifanya Jeshi hilo kuafanya uchunguzi wa kina ni Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, mbunge wa Same Mashariki (CCM), Bibi Anne Kilango, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya IPP na Bw. Reginald Mengi.

  Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari vinavyofahamu kwa kuna upelelezi huo, uchunguzi huo umepata nguvu baada ya Bw. Mengi ambaye juzi alitangaza hadharani kutishiwa kuuawa na Waziri aliyemtaja kuwa kijana na msomi, kuwasilisha rasmi malalamiko polisi na ushahidi wa ujumbe mfupi wa simu ambao pamoja na kutishiwa yeye kupitia ujumbe huo, pia walishiwa kuuawa kwa sumu Spika, Mama Kilango, Dkt. Mwakyembe na Bw. Kubenea.

  Bw. Mengi, kwa mujibu wa taarifa za polisi, aliripoti rasmi tishio hilo Septemba 24 mwaka huu na kufungua kesi ya kutishiwa maisha.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu hivyo, ujumbe ambao umewatishia viongozi hao na Bw. Kubenea ambao Mengi aliuwasilisha polisi unasomeka hivi: ''Sitta taarifa ulioitoa haisaidii wewe na wenzio Mengi, Kubenea, Mwakyembe na Kilango mtauawa tu kila kitu kiko katika mstari, (John) Malecela (mbunge wa Mtera CCM) mwambie mkeo (Anne Kilango).

  " .....(ujumbe huo unamtaja mfanyabiashara mmoja) alituma vijana wawili UK (Uingereza) kutafuta sumu aina ya RICIN ambayo inaweza kuua ndani ya saa 48, vijana hao waliuawa na wanausalama wa mataifa makubwa duniani kwani walidanganya sumu hiyo ni ya kumuua Balozi wa Taifa moja wakidhani wakisema hivyo watauziwa.''

  Majira lilifanikiwa kufanya mahojiano na baadhi ya viongozi waliotajwa kwenye ujumbe huo ambao walithibitisha kupokea vitisho kama hivyo kwa nyakati tofauti.

  Spika wa Bunge, Bw. Sitta alisema taarifa za vitisho hivyo zilitolewa kwa viongozi mbalimbali kulingana na misimamo yao katika vita dhidi ya ufisadi nchini.

  Alisema Agosti mwaka huu, alitumiwa ujumbe wa aina hiyo akitishiwa maisha yake na alilazimika kuwasiliana na walinzi wake ambao walikwenda kutoa taarifa za vitisho hivyo Polisi.

  "Simu tunazopigiwa na ujumbe tunaotumiwa katika simu zetu ni uhalifu wa kisiasa hivyo ni wajibu wa Jeshi la Polisi kuchunguza taarifa hizi kwa mtu yeyote anayetishiwa maisha yake," alisema Bw. Sitta.

  Bw. Sitta alisema, vitisho alivyowahi kutumiwa havimpi wasiwasi kama inavyochukuliwa na wahusika wa uhalifu huo, bali ataendelea kusimama katika misingi ya kazi yake kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

  Naye Dkt. Mwakyembe alipoulizwa kwa njia ya simu jana alisema msimamo alionao katika vita dhidi ya vitendo vya ufisadi nchini, umemjengea uadui na kupata vitisho tofauti kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi.

  Alisema vitisho vya aina hiyo, pia vilitolewa kwa viongozi wengine ambao walionesha misimamo yao katika suala hilo lakini vitisho hivyo, sio kigezo cha kuwafanya viongozi hao kushindwa kutetea maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

  Alipotakiwa kuelezea baadhi ya maneno yaliyokuwa katika ujumbe ambao Bw. Mengi amelazimika kuuwasilisha polisi, Dkt. Mwakyembe alisema, vitisho hivyo vilitolewa muda mrefu na kusisitiza kuwa polisi wanataarifa juu ya vitisho hivyo.
   
Loading...