Polisi waache kutumika kunyanyasa wadaiwa

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
614
Tatizo la wizi wa kuaminiwa ni kubwa na baya linawaumiza wengi, lakini tatizo la polisi wetu kutumiwa vibaya na wenye pesa kugeuza kesi ya madai kuwa jinai kwa kisingizio ni wizi wa kuaminiwa nalo ni kero zaidi hasa kwa wananchi wanyonge na masikini ambao wanasumbuliwa na polisi na kuwekwa mahabusu wakijikuta wanadaiwa na matajiri hata kama walikopeshwa ama walipata hasara katika biashara zao.

Leo nimepata mfano wa pili katika kipindi cha wiki mbili namba tutafakari kwa pamoja;

Jana usiku wa kuamkia leo 7/4/2016 saa 6.30 (00.30) polisi mmoja wa kiume kutoka kituo cha Sitaki Shari bila kujitambulisha wala bila kuwa na kiongozi wa mtaa alikwenda Majohe nyumbani kwa mama mmoja aitwaye Joha Gulam na kumchukua kwenda naye kituoni.

Polisi aligonga mlango na alipofunguliwa akaulizia yule Mwanamke huyo alipotoka akachukuliwa bila hata maelezo na bila hata kumwambia mumewe.

Mume wa Joha alipowafuata akawakuta wanataka kuondoka na gari moja ya kiraia. Mumewe Joha aitwaye Ramadhani alitambua abiria wengine katika ile gari kuwa ni wanawake ambao waliwahi kuwa waajiri wa mkewe na yule polisi akamwambia asijisumbue kuwafuata akalale aende polisi kukishakucha.

Ramadhani ameenda leo asubuhi akiwa na nyaraka ajili ya dhamaba amefukuzwa na kuambiwa aende jioni saa 10 kwani saa hizi hawatoi dhamana.

Maelezo ya Ramadhani ni kwamba zaidi ya miezi kadhaa iliyopita wanawake aliowaona na polisi waliwahi kulalamika kwamba wanamdai Joha fedha zilizosemekana walipata shoti katika biashara ya duka alilokua akiuza Joha lakini baada ya mashauriano ya muda mrefu suala hilo walilimaliza na mkewe na mkewe akawa anafanya shughuli zake nyingine.

Hoja hapa ya kujiuliza ni kwanini wamemchukua usiku wakati anayo sehemu ya biashara anayofanyia kazi kila siku? Kwanini madai yao yamegeuzwa kuwa jinai?

Kesi hiyo inafanana na kesi nyingine mkoani Mbeya ambayo mzee mmoja aliyekopa kwa mwenzake na anakabidhi hati ya nyumba alivyokamatwa na kukaa polisi kwa zaidi ya wiki mbili kwa maelezo ya anayemdai na polisi walikua wakisema hawawezi kumuachia hadi anayemdai awape maelekezo.


Kesi hiyo ya Mbeya iliingiliwa na wakuu wa polisi na kufanikiwa kufikishwa mahakamani ambako nako kuna majipu mengine hasa mahakama zetu za chini na zaidi mikoani na pembezoni.

Je, hakuna sheria ya polisi wenyewe ila mwenye mali ndiye anawapangia nini cha kufanya? Je, ni kwann watu wanaodai na ambao hawajatendewa jinai watumie polisi kunyanyasa watu na wakati mwingine kuwadhulumu?
 
Back
Top Bottom