Polisi Shinyanga wanamshikilia baba kwa kumbaka binti yake wa miaka mitatu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
shinyanga.gif

Jeshi la polisi wilayani Kishapu Shinyanga limemtia mbaroni mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ngasa Sekwa mkazi wa Maganzo Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka mitatu na kumjeruhi vibaya sehemu zake za siri.

Akithibitisha tukio hilo kwa niaba ya Mkuu wa kituo cha Polisi wilayani Kishapu Kaimu mkuu wa kituo cha Polisi cha Maganzo Afande Oscar Shani amekiri kuwa baada ya mtuhumiwa kukamatwa mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amefanyiwa uchunguzi wa kitalaamu na kubainika kuwa amebakwa na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri ambapo pia walimuuliza maswali na kumtaja baba yake kumfanyia kitendo hicho.

ITV ilifika katika kituo cha Polisi cha kishapu ambapo mtuhumiwa amewekwa rumande akisubiri kufikishwa mahakamani na kufanikiwa kuzungumza naye ambapo amekataa kuhusika na kitendo hicho huku Bi.Milembe Luhende ambaye ni bibi wa mtoto huyo akidainkuwa mtuhumiwa alikuwa akimfuata mtoto kila siku na kwenda naye nyumbani kwake na kisha kumrudisha jioni ambapo siku moja alimuona mjukuu wake akiwa tofauti ndipo alipochukua hatua ya kumchunguza na kukuta anatokwa na uchafu katika sehemu za siri.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi.Hawa Ng’humbi ambaye alifika kushuhudia tukio hilo amevitaka vyombo vya dola kutoichezea kesi hiyo nakutaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine kwakuwa katika kipindi cha miezi sita matukio matano ya ubakaji wa watoto wilayani humo yamesharipotiwa.

Chanzo: ITV
 
Binti wa miaka mitatu???...................... he!

wakati nikivikataa vi-ke vya 18-20 nikiona bado vitoto kumbe kuna watu watu akili za bata hivi? wanaharisha kila sehemu!! daah...

Uganga na uchawi upite mbali
 
shinyanga.gif

Jeshi la polisi wilayani Kishapu Shinyanga limemtia mbaroni mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ngasa Sekwa mkazi wa Maganzo Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka mitatu na kumjeruhi vibaya sehemu zake za siri.

Akithibitisha tukio hilo kwa niaba ya Mkuu wa kituo cha Polisi wilayani Kishapu Kaimu mkuu wa kituo cha Polisi cha Maganzo Afande Oscar Shani amekiri kuwa baada ya mtuhumiwa kukamatwa mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amefanyiwa uchunguzi wa kitalaamu na kubainika kuwa amebakwa na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri ambapo pia walimuuliza maswali na kumtaja baba yake kumfanyia kitendo hicho.

ITV ilifika katika kituo cha Polisi cha kishapu ambapo mtuhumiwa amewekwa rumande akisubiri kufikishwa mahakamani na kufanikiwa kuzungumza naye ambapo amekataa kuhusika na kitendo hicho huku Bi.Milembe Luhende ambaye ni bibi wa mtoto huyo akidainkuwa mtuhumiwa alikuwa akimfuata mtoto kila siku na kwenda naye nyumbani kwake na kisha kumrudisha jioni ambapo siku moja alimuona mjukuu wake akiwa tofauti ndipo alipochukua hatua ya kumchunguza na kukuta anatokwa na uchafu katika sehemu za siri.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kishapu Bi.Hawa Ng’humbi ambaye alifika kushuhudia tukio hilo amevitaka vyombo vya dola kutoichezea kesi hiyo nakutaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine kwakuwa katika kipindi cha miezi sita matukio matano ya ubakaji wa watoto wilayani humo yamesharipotiwa.

Chanzo: ITV
wasukuma bwana sijui wana tatizo gani
 
Wampime kwanza akili...bila shaka ubongo wake utakuwa umecheza kidogo sababu hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kufanya huo ujinga...!vinginevo amfichue mganga aliyemtuma...!
 
Hapo wanaohusika kwa uhakika waganga wa kienyeji,napata wasiwasi kama watu wa aina hii wakawa wazazi,mbona kawaida Mungu kaweka upendo wa uhakika kwenye mioyo ya wazazi kwenda watoto ,
ajabu unaoana mzazi anaweza kufanya unyama huu kwa mtoto wake naona ajabu sana
 
Back
Top Bottom