Polisi na wanajeshi wa majeshi yote nanyi ni Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na wanajeshi wa majeshi yote nanyi ni Watanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jibaba Bonge, Oct 23, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tukiwa tunakaribia siku ile ya uchaguzi mkuu, ninawiwa kuwakumbusha ndugu zetu polisi na wanajeshi wa majeshi yote kuwa wao pia ni watanzania. Siku ile wasije wakakubali kutumiwa kwa faida ya wachache.

  Makundi haya niliyoyataja ni mgawanyo wa kazi tu kama walivyo walimu, wakulima, wafanyakazi wa maofisini, wafanyabiashara n.k. Ugumu wa maisha na athari za ufisadi zinazotukabili watanzania hazijabagua haya makundi.

  Ombi langu kwa polisi na wanajeshi- kumbukeni kuwa na nyinyi ni watatnzania msikubali kutumiwa na watu wachache ambao tena hawatakuwa mstari wa mbele kama nyinyi maana wao wataawagiza ninyi kutekeleza matakwa yao wakiwa maofisini tena wakilindwa na nyinyi wenyewe. IWENI SEHEMU YA MABADILIKO, KATAENI KUTUMIWA, TEKELEZENI MAJUKUMU YENU KWA HAKI, KUWENI NA UCHUNGU NA NCHI NA WANANCHI WA TANZANIA SIO MATAKWA YA KIKUNDI KIDOGO CHA WATU KWA FAIDA YAO BINAFSI.

  KUMBUKENI SIKU YA 31 OKTOBA 2010, MUWE SEHEMU YA HISTORIA NZURI YA TANZANIA
   
Loading...