Salamu.
Nimesoma na kusikiliza kwa masikitiko maelezo waliyoyatoa familia ya Allen kijana wa miaka 20 mfanyabiashara ndogo ndogo aliyeuawa bila kosa lolote na polisi wa Mbeya.
Hakuna shaka tulipofikia tumefikia pabaya, mauaji ya ovyo ovyo, kamata kamata ya ovyo ovyo, vitisho na upotevu wa raia wasio na kosa lolote na uvunjaji wa wazi wa haki za binadamu.
Tulitegemea polisi watulinde wananchi na mali zetu lakini hao hao ndiyo wa kwanza kutuua, kweli tunapokwenda si sahihi hata kidogo. Huyu waziri Mwigulu naona ameshalewa na hajui analofanya, dhaifu, muonevu, muuaji, mtekaji na amejaa kila aina ya uovu.
Suala la huyu kijana Allen alivyouawa kirahisi inasikitisha sana, mauaji yake ni muendelezo wa mauaji mengi ya wananchi wasio na hatia chini ya Serikali ya dikteta uchwara Magufuli.
Nimeanza kuamini kifo katika nchi hii ni rahisi sana...Siyo tena bwana ametoa, bwana ametwaa! Ni mauaji kwa kwenda mbele, yana mwisho haya, siku moja tutawaona Magufuli, Mwigulu, makonda na wengine huko TISS na usalama wa taifa kwa ujumla mkijibu mashtaka kwa yote mliyoyafanya na mnayoendelea kufanya!
Mnaua vijana wadogo wasio na hatia, kwanini? Wamewakosea nini? Mkumbuke hayo mauaji, utekaji, na mateso mnayowatendea watanzania wasio na hatia yanaingia kwenye rekodi, hayataishia kwenye magazeti tu.Leo mtafurahia lakini mtakuja kujibu baadaye!
Nchi imeshakuwa ya sarakasi tupu kwa sababu inaongozwa na washamba na malimbukeni wasiojua wanafanya nini. Hivi wazazi wenu(Magufuli, Mwigulu, Sirro, Kipilimba na Makonda) wako proud kuwa na watoto kama ninyi?
Sarakasi inaendelea.Juzi wamempandisha aliyemtolea Nape Nnauye bastola kama mmoja wa washtakiwa kwenye gari lililowabeba viongozi wa chadema waliokuwa wakipelekwa gerezani wakati huo huo mwigulu aliji-contradict kuwa huyo si askari na bado wanamtafuta?......Hivi credibility gani mnayo kudanganya waziwazi tena bila wasiwasi?
Kuna siku wanaoonewa watachoka halafu hali itakuwa mbaya, tanzania ni yetu sote. Si ya wana ccm na wanaojikomba komba kwa Magufuli
Credit:
field marshall1