DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Ileje, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Kisbert Kapondo, ametoa elimu kwa waendesha bodaboda wa Kata ya Itumba Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe akiwataka kuepuka kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Akizungumza Oktoba 19, 2025 na wasafirishaji hao katika kijiwe chao, ASP Kapondo aliwaeleza kuwa wao ni wadau muhimu wa usalama barabarani na maendeleo kwa jamii, hivyo wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kutii sheria na kudumisha amani, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
Aidha, ASP Kapondo aliwasihi wasitumika na watu wenye nia ovu wanaotaka kuvuruga amani kwa kutumia wao kama nguzo ya chombo cha uchochezi, huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayebainika kushiriki kwenye uvunjifu wa amani au kuvunja sheria kwa njia yoyote ile.